Haini ni mtu gani? (Mithali 13:2)

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 13:2 “Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri”

Haini au Kwa lugha nyingine tunaweza sema MSALITI, Hivyo haini ni mtu msaliti ambaye hufanya usaliti kwa mtu fulani, au mtu anayefanya usaliti katika nchi yake kinyume na uzuri wa jambo fulani

Lakini pia hata katika Imani mtu anayesaliti Imani itakayompeleka mbinguni kwa yale tunayo yaona ni mema tukiwa ndani ya Kristo Yesu na Kufanya kinyume/kunena kinyume inafanishwa pia haini au msaliti

maandiko yameonyesha jambo hilo
Zaburi 78:57 “Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakaepea kama upinde usiofaa
58 Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao.
59 Mungu akasikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa.”.

Na maandiko yanazidi kuonyesha kuwa Wahaini wote wa imani watapata adhabu..

Zaburi 119:158 “Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako”.

Mithali 22:12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.”
Soma pia Mithali 13:15 na Zaburi 25:3.

Ni nini basi cha kuzingatia katika maisha yetu, lazima tuwe na msimamo thabiti tusiwe haini mbele za Mungu, tusimtaje Mungu Kwa midomo yetu, alafu mioyo yetu ikiwa mbali naye, kama umeamua kumfuta Mungu basi kubari kuachana na yote ya ulimwengu huu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa kuishi maisha yapatanayo na toba uliyoifanya, na ishi kulingana na neno la Mungu linavyosema, usiwe vuguvugu watu wenye tabia kama hii Mungu hapenzwi nao, MBELE ZAKE WANAONEKANA KAMA WASALITI, Kwa sababu wanalijua neno lakini hawaliishi, Kwa kuwa umekombolewa ishi kama Mtu unayekomboa wakati, ukiithamini nguvu ya masalaba

Na ikiwa bado ujaokoka, basi wakati ni huu maana huwezi kuishinda dhambi nje ya Kristo, mwamini Leo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *