MAPEPO NI NINI?

  Maswali ya Biblia

Mapepo ni roho au malaika walioasi mbinguni, walishindwa kuilinda Enzi yao mbinguni(Yuda 1: 6)wakaingia tamaa na kushawishiwa na Shetani (pia nae alikuwa ni malaika) na kutaka kuupindua ufalme wa Mungu lakini hawakufanikiwa wakafukuzwa.

Hivyo mkuu wao anaewapa amri na kuwaongoza hawa mapepo ni Shetani yeye ndio pepo mkuu.

Hivyo baada ya kuasi wakatupwa huku chini na kipindi wanaasi na kufukuzwa Mwanadamu alikuwa bado hajaumbwa.

Baada ya Mwanadamu kuumbwa ilibisi alipofanikiwa tu kumdanganya Mwanadamu na kumuangusha pale Edeni kila kitu kilibadilika na Mapepo yakapata nafasi ya kuingia katika Mwili wa Adamu na kufanikiwa kuleta uharibifu wa kila namna na yakapata mamlaka ya kufanya kama yapendavyo hapa duniani.

Hivyo baada ya Mwokozi kuja Dunia Yesu Kristo mapepo yalinyang’anywa mamlaka kubwa yaliyokuwa nayo hapa duniani. Na Yesu ndio akamchukua hayo mamlaka ambayo Shetani aliyachukua kwa Adamu. Na mamlaka hayo tukapewa sisi pia tuliomwamini Yesu Kristo.

Ufunuo 1:17 “…………Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”.

Hivyo Mapepo yote(theruthi ⅓ malaika walioko mbinguni). Yaliyopo hapa duniani hayana nguvu tena na mamlaka kwa Mtu aliemuamini Yesu Kristo hayawezi chochote ni dhaifu kabisa ila kwa mtu alie nje ya kristo mapepo yananguvu kwake na yanaweza kufanya lolote. Soma (Mathayo 28:28).

Hivyo Shetani hapo zamani alikuwa na uwezo wa kwenda kwa wafu waliokufa na akafanya chochote alichoona chema akilini mwake jambo ambalo huko nyuma alikuwa hana mamlaka hiyo…

Ukisoma kitabu cha Samweli utaona baada ya Samweli kufa na Sauli Mfalme alikuwa akitaka kuzungumza nae yule mwanamke mchawi aliweza kumpandisha Samweli juu ili azumgumze na mfalme Sauli. Hivyo mamlaka hayo yote Yesu Kristo alimnyang’anya Shetani na mtu akifa Shetani hawezi kumfikia huko aliko wala hawezi kufanya lolote juu yake.

Yako Mapepo ya namna mbali mbali hivyo ikiwa uko nje ya Kristo jua kabisa unamapepo huenda unajiuliza kivipi sasa? Na sijawahi kulipuka mapepo ndugu unayo si mapepo yote yanalipuka.

Mengine ni ya magonjwa.(Luka 13:11)

Mengine ni ya mateso/mkandamizo wa nafsi, mpaka kupelekea kujiua. Mf. Ndio Yule alimwingia Yuda ikampelekea kwenda kutenda dhambi na kujinyonga.

Mengine ni ya utambuzi: (Matendo 16:16)

Mengine ni mapepo bubu na kiziwi;(Marko 9:25)

Mengine ni ya kukudanganya.(1Wafalme 22:22).

Yapo Mengine mengi sana yanayowavaa wanadamu…

Hivyo kama upo nje ya Kristo fahamu kabisa unamapepo na njia pekee ya kuyaondoa hayo ni wewe kumpa Yesu Kristo maisha yako kwa kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO na baada ya hapo utapokea Roho Mtakatifu. Hapo ndipo utaanza kuona badiliko jinsi ulivyo na ulivyokuwa utaona tofauti kubwa sana.

Tumepewa Amri tunapomwamini Yesu Kristo.

Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru

Hizi ni siku za Mwisho hizi Shetani anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha unaenda kuzimu kama usipokuwa tayari kuyakabidhi maisha yako kwa Yesu utaenda na Shetani motoni milele.

Shetani anajua muda wake ni mchache na anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha anakwenda na watu wengi kuzimu ikiwemo wewe hapo kama hujampa Yesu maisha yako.

Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu’.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT