Nini Maana ya Kongwa?.

Maswali ya Biblia No Comments

Kongwa ni nira au kifungo cha shingoni ambacho kinatengenezwa kwa kutumia mti uliogawanyika sehemu mbili au mti uliochongwa unaoshikamanisha au kuunganisha vitu viwili katika sehemu moja.

Mfano Ng’ombe wawili wanaofungwa pamoja shingoni kwenda kulima kwa kutumia pilau(jembe la ng’ombe la kulimia) Na pia hata kwa watu zamani walikuwa wakifungwa nayo katika kipindi cha biashara ya utumwa. Watumwa waliokuwa wakionekana kutaka kutoroka au wananguvu walikuwa wanafungwa Komgwa mstari wa watu hata 10 hiyo inafanya kuwa ni ngumu wao kutaka kukimbia au kuleta fujo.

Katika Biblia Kuna sehemu nyingi neno hili tunalisoma…

Kumbukumbu la Torati 28:48 “kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza”.

Soma pia…

Matendo 15:10 “Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua”.

Wagalatia 5:1 “Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa”.

Walawi 26:13 “Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa”.

1Wafalme12:4 “Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia”.

Na sehemu mbali mbali kama ni msomaji wa Biblia utakutana nalo neno hili.

Kongwa katika agano la Kale linafananishwa na Sheria ile iliyokuja kwa mkono wa Musa ambayo kwa wana wa Israeli na kwa mtu yoyote mwenye mwili ilionekana kuwa ni nzito sana, hawakuweza kuendana nayo na hata wengi waliangamizwa. Na Mafarisayo walikuwa wakiwafungia watu Makongwa kwa kuongeza mambo hata ambayo hawakuweza kufanya.

Sasa Je!, sisi katika agano jipya tuko katika Kongwa lipi? Na Je tuko katika Kongwa lipi la Mungu au la Shetani?.

Kwa ambao tuko katika Neema ya Kristo tuko katika Kongwa la Roho Mtakatifu yaani tuko chini ya Sheria ya uzima ambayo iko katika roho zetu. Hatuko katika Sheria ya uzima na mauti.

Lakini ikiwa mtu yuko nje ya neema ya Kristo huyo Mtu yuko chini ya kongwa la Shetani na anamtumikisha jinsi anavyotaka na mwisho wa siku ni mauti.

Ikiwa bado hujaokoka usisubili mpaka muda ufike muda tayari umeshafika na ndio huu tuko mwishoni kabisa hujachelewa bado unayo nafasi ya kutengeneza mambo yako na Kristo leo wala si kesho..

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *