Marhamu Ni Nini? Na Manukato Ni Nini?

Maswali ya Biblia No Comments

Marhamu, ni kimiminika kilichotengenezwa kutokana na mimea mbalimbali ili kufanya kitu kiwe na harufu nzuri na kufukuza wadudu na viumbe waharibifu, aya Kwa Jina lingine ni pafyumu

Lakini viwango na ubora wa manukato hutofautiana, kukiwa na marhamu ya bei ghali ambayo hayapunguzi harufu haraka, kama yale yaliyotumiwa na Yesu huko Bethania yalikuwa na ghali kwa kiasi kikubwa. na pia utaona Maria Magdalene na wengine walitayarisha marhamu kwa ajili ya kumpaka Bwana siku ya kwanza ya juma.

Mathayo 26:6 “Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,
7 mwanamke mwenye KIBWETA CHA MARHAMU ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.
8 Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?
9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini”.

Na

Manukato ni viungo ambavyo vinapochomwa, kupikwa, au kuwekwa mahali fulani, hutoa harufu fulani inayovutia au kuwakilisha kitu Fulani lakini havipo katika hali ya kimiminika,. Mifano ya manukato ni pamoja na UDI, UVUMBA, na MANEMANE.

Zipo marhamu ambazo ni ghali na huuzwa kwa gharama kubwa na hudumu, na zipo zingine ni ya gharama nafuu lakini huwa harufu yake haidumu kwa muda mrefu katika mwili wa mwanadamu.

Luka 23:56 “Wakarudi, wakafanya tayari manukato na MARHAMU. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa”.

Nasi pia yatupasa tufanyike marhamu na manukato kwa Bwana kwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kama vile Kristo alivyokuwa kielelezo kwetu, maisha yetu yasiye harufu mbaya bali tukawe marhamu yenye viwango vya juu, tukiikataa Dunia na mambo yake yote na kuishi maisha yenye harufu nzuri, tukidumu katika utakatifu, maombi, na Ibada

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *