Je! Sabato halisi ni ipi? Ni jumapili au Jumamosi? Ni siku gani sahihi ya kuabudu?.

  Maswali ya Biblia

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Tukisoma katika maandiko Matakatifu Neno la Mungu linasema

Yohana 4:24″Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”.

Mkristo yoyote aliekombolewa kweli kweli na Damu ya Yesu Kristo hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa kushika siku,mwezi,Mwaka, kwa kuabudu. Hatuhesabiwi haki katika hayo!.

Kuabudu Jumamosi, Jumapili, Jumatano, ijumaaa nk huo ni utaratibu tu wa watu wamejiwekea wakusanyike wote sehemu fulani na siku fulani kwa ajili ya kumuabudu Mungu kwa pamoja kama Neno lilivyoagiza.

Waebrania  10:25″wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.”

Neno linasema “WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA….” halijasema “SIKU FULANI MSIACHE KUKUSANYIKA”.

lakini anasema “..kama ilivyodesturi..” maana nyingine ya desturi ni Utaratibu.

Hivyo utaratibu huo haumuongezei mtu chochote katika roho. Hakuna siku maalumu kuwa Mungu anatusikiliza katika hiyo. Na siku nyingine hatusikilizi, bali siku zote Mungu anatusikiliza.

Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”

Kuendelea kushika siku,miezi na miaka ni kuonyesha kuwa mtu anaefunya hivyo bado hajamjua vyema Mungu.

Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”  

Sasa Sabato ni nini?? Maana yake ni PUMZIKO. Na pumziko letu la kweli Wakristo liko katika roho na si katika mwili tena kama ilivyokuwa hapo awali katika agano la Kale.

Ukisoma pia utaona kuwa Bwana wetu Yesu Kristo ndio Bwana wa Sabato.

Mathayo 12:8″Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.”

Hivyo ukiokoka ukampata Kristo ndio umeipata sabato Yenyewe halisi katika Roho maana yeye atakupumzisha na kila aina ya mizigo uliyonayo.

Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Hivyo anaeabudu Jumamosi, Jumapili, Alhamis,Jumatano nk hawafanyi kosa kabisa mbele za Mungu maana Mungu haha hajachagua siku fulani ndio aabudiwe na ndio atatusikiliza sivyo!, yeye tunamwabudu katika Roho na kweli na si katika siku.
Hivyo tunaposoma Biblia

Wakristo wa kwanza(Kanisa la kwanza la Mitume) walichagua siku ya Jumapili kwa ajili ya kukusanyika,kumega mkate na kufanya Changizo (Matendo 20:7, 1 Wakorintho 16:1-2)utaona jambo lile lile maandiko yanasema.

Hivyo Mungu anaabudiwa katika Roho kila saa kila wakati na popote pale iwe chini ya mti nk.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT