Safina ni nini?

  Maswali ya Biblia

Safina ni chombo cha majini kilichotumika kuokoa, yaani kipo mahususi kwa ajili ya okombozi endapo tatizo litatokea ,Kwa lugha ya kiyahudi hiitwa  “Tevat”,  tukisoma katika maandiko Kipindi cha Nuhu, wakati Mungu alipotaka kungamiza dunia, Mungu alimpa Nuhu maagizo ya kutengeneza safina ambayo ataingia yeye pamoja na familia yake, na wanyama ambao Mungu alivuta waingia Kwa ajili ya kutunza uzao, lengo la Mungu lilikuwa kwa ajili ya kuwaokoa na ghadhabu inayokuja

Mwanzo 6:13-14
13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.

Dhumuni kuu la safina lilikuwa kwa ajili ya kuokoka, ni mfano wa meli ambayo hutumika kwa ajili ya kuokoa endapo tatizo linapotokea.

Na ilikuwa ili safina kamilike ni  lazima ipakwe lami ndani na nje, lami ni mfano wa gundi nzito, ambayo kazi yake lami ilikuwa kwa ajili ya kuzuia maji yasiingie ndani,
Na ndiyo maana Mungu alivyokuwa anampa Nuhu maagizo ya kujenga safina alimwambia juu ya hilo “ukaifunike nje na ndani Kwa lami”
kwahiyo lami ilisaidia maji kutopita kabisa hata yawe mengi kiasi gani.

Je hii safina inafunua Nini?
Safina ndiye Yesu Kristo, yeye ndiye mwokozi wa maisha yetu, maandiko yanasema ” ili Kila amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele, hivyo hakuna ukombozi nje ya Yesu, yeyote aliye nje kupata na dhoruba ni rahisi,
na  lami ambayo ilikuwa inapakwa nje na ndani ilikuwa inawakilisha DAMU YA YESU, ambayo ilimwagika Kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, ambayo inanena mema katika maisha yetu, na inatuepusha na ghadhabu ya Mungu juu ya maisha yetu

Warumi 8:1-2
1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Huu si mda wa kucheza cheza, ni mda wa kuomboa hatima ya maisha yako maana lengo kuu la Mungu kwetu si kutuangamiza Bali kutukomboa ndiyo maana akatuletea njia iturudishayo kwake, Sasa ukikataa na njia hii una tarajia Nini
Mwamini Leo Yesu ili uwe na amani na uhakika wa maisha yako.

ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT