Nini maana ya KK na BK?.

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

KK na BK ni vifupisho vinavyotumika kuonyesha nyakati mbali mbali.

KK. Ni kifupisho kinachomaanisha “Kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo”  yaani (B.C Before Christ) kwa kiingereza. Hivyo sehemu yoyote unapoona pameandikwa KK Maana yake wakati huo Kristo alikuwa bado hajazaliwa.

B.K Ni kifupisho cha wakati chenye maana ya “Baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.” Kwa Lugha ya kiingereza ni (A.D Anno Domino) ni neno la kilatini lenye maana ya “Anno Domino-in the year of the Lord maana yake ni KATIKA MWAKA WA BWANA”.

Hivyo mahali popote unapokuta mwaka umeandikwa mbele yake AD inaonyesha katika wakati huo Masihi, Yesu Kristo alikuwa ameshazaliwa.

Lakini katika dini zingine ambao wao si Wakristo waaamini katika dini zao utakuta wanaandika K.W.K  “maana yake ni Kabla ya wakati wa kawaida” kwa kiingereza ni B.C.E – Before the  common Era. Lakini hii haina tofauti na K.K

Pia W.K ikiwa na maana ya wakati wa kawaida. Kwa Lugha ya kiingereza ni Common Era.(C.E).

Hivyo unapokuta mahali popote iwe ni katika hostoria labda kitabu cha Isaya kiliandikwa kati ya 681 na 701 KK. Maana yake ni kitabu ambacho kiliandikwa kabla Masihi hajazaliwa Duniani .

Na unapokuta labda kitabu cha UFUNUO kiliandikwa kati ya mwaka 90 na 95 Bk maana yake kiliandikwa Kristo alikuwa tayari ameshazaliwa mpka mwaka 2000+ bado ni BK. Si toka iumbwe lakini tangu Kristo afe na kukufuka kwake.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT