YESU ALIZALIWA WAPI?

  Maswali ya Biblia

Ukiwa kama mwamini mambo kama haya huna budi kujifunza na kuelewa ili yazidi kukuimarisha na kukujenga kiroho…

Tukirudi kwenye swali letu linalosema Yesu alizaliwa wapi..Bwana Wetu Yesu Kristo alizaliwa katika Nchi/Taifa la ISRAELI, lililopo mashariki ya kati. Na mji aliozaliwa ni Bethlehemu ambao ulikuwa katika urithi wa kabila la YUDA…

Mika 5:2 “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”.

Ijapokuwa Bwana Yesu alizaliwa Katika Bethlehem kulingana na kile nabii mika alichokitabiri lakini tunakuja kuona  wazazi wake hawakukaa sana huko bali waliishi mahali palipojulikana. NAZARETI

Mji mdogo sana uliopo kaskazini mwa Taifa hilo la Israeli, na huko ndiko Kristo alikokulia, ndio maana mahali pengine anajulikana kama Mnazorayo (yaani mtu wa Nazareti).

Mathayo 2:23 “akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo”.

Ndani ya mji huo wa nazareti ndipo kuna wilaya iitwayo Galilaya, mji wa Bethlehemu aliozaliwa Bwana YESU ulikuwa katika Wilaya iliyoitwa Yudea au Uyahudi

Na ndani ya wilaya ya Galilaya Ndipo utaona kuna miji mingine midogomidogo kama Kapernaum, korazin, Bethsaida, na ndo miji ambayo wanafunzi wengi wa Bwana Yesu walitokea huko, miji hii ndio hiyo iliyoshuhudia miujiza mingi aliyoifanya Bwana Yesu lakini haikutaka kutubu (Mathayo 11:21)…Wilaya ya Uyahudi ndio iliyobeba miji ya Bethlehemu pamoja na Yerusalemu.

Kwa uhalisia ni kwamba Bwana Yesu alizaliwa Bethlehem ya uyahudi akakulia Nazareti ya Galilaya, na alikufa hapo Yerusalemu na kuzikwa huko huko na kufufuka YERUSALEMU, lakini sasa yuko hai  anatawala,na atarudi tena mara ya pili kuwachukua watu wake..siku zimekaribia sana Maaandiko yapo wazi…

Je umeokoka?

Bwana YESU ANARUDI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT