Liwali ni nani?

Maswali ya Biblia No Comments

Liwali ni mkuu wa mji au jimbo fulani au Kwa maana nyingine anajulikana kama Gavana

Mfano Katika biblia tunamsoma Yusufu, farao alimfanya kuwa liwali katika nchi yote ya Misri

Mwanzo 42:6

6 Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.

Na kazi yao kuu, ya hawa mawaliwali ilikuwa Kwa ajili ya kusimamia, na kuongoza shughuli zote za jimbo au mji huo kwa mamlaka yao, maana hakuna chochote kinachoweza fanyika bila ruhusa yao, mfano kwa kipindi hiki tunaweza kuwaita wakuu wa mikoa.
na walikuwa na uwezo wa kufanya hukumu Kwa mtu yoyote anayeenda kinyume na taratibu na sheria  waliyoweka , ndiyo maana wakati Bwana Yesu anaenda kusubiwa tunaona alipekwa pilato aliye liwali

Mathayo 27:1-2
1 Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.

Japokuwa hawa maliwali, yanayo mamlaka ya kufanya chochote, lakini lipo jambo la kujifunza ambalo Bwana alitaka tulifahamu
Bwana Yesu aliwazungumzia hawa ili kutupa ujasiri sisi watumishi, endapo kama  tukiwekwa mbele yao Kwa ajili ya kutushtaka tufanye Nini?

tusome

Mathayo 10:18-20

18 Nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.

19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.

20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu

Inawezekana  katika kazi ya utumishi wetu, kuna wakati utafika tutawekwa mbele yao kwa ajili ya jina lake, kushtakiwa Kwa sababu ya kuifanya kazi ya Injili, lakini Bwana anatuambia katika hayo yote hatupaswi kuogopa Wala kujiuliza tutajibu Nini tukiwekwa mbele yao, usiwe na shaka. Katika kuifanya kazi ya Bwana, itende Kwa ujasiri maana Bwana yupo pamoja nawe

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *