Mtu aliyeishi miaka mingi duniani ni nani?

  Maswali ya Biblia

Maandiko yanaeleza wazi juu mtu aliye ishi miaka mingi katika biblia ukisoma

Mwanzo 5:25 “Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.

26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.

27 Siku zote za Methusela ni miaka MIA KENDA NA SITINI NA KENDA, AKAFA”.

Methusela Mwana wa Henoko aliyetwaliwa na Mungu, kulingana na maandiko methusela ndiyo mtu aliye ishi miaka mingi zaidi kuliko wote, maana miaka aliyoishi ilikuwa miaka 969, wapo na baadhi walioishi miaka mingi lakini hawakuifika ya methusela
unaweza pitia vifungu hivi kwa mda wako
(mwanzo 5:20, mwanzo 9:29, mwanzo  5:5, mwanzo 5:14, mwanzo 5:11).. nk

Lakini kuna jambo lilioneka kuhusu miaka ya wanadamu, baada ya Gharika kapindi Ndugu, tunaona miaka ya wanadamu ilishushwa, hadi kufikia miaka 120, na hii ilikuwa si kwa wote wengine walikufa hata kabla hawajafikisha miaka hiyo soma (mwanzo 6:3)

Kwa jinsi tena siku zilivyokuwa zinakwenda miaka ikazidi kupungua  kutoka 120 hadi 80
Zaburi 90:9 “Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.

10 Siku za miaka yetu ni MIAKA SABINI, NA IKIWA TUNA NGUVU MIAKA THEMANINI; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara”.

Je  jambo hili  linasababishwa na nini, kwanini miaka ya kuishi inazidi kupungua?

Kuna mitazamo mingi kuhusu swali hili, wengi hudai kuwa ni kwa sababu ya vyakula tunavyokula vimezidi kemikali (madawa), watu hawazingatii lishe hawali. chakula bora, na hawali kwa wakati ndiyo maana inasababisha kufa mapema, wengine husema Kwa sababu watu hawafanyi mazoezi, au hali ya hewa, na  ipo mitazamo mingi, Ni kweli kibinadamu kwa asilimia chache inaweza ikawa hivyo, lakini kiuhalisia mbele za Mungu mambo haya hayana ukweli wowote.

Jambo linalopelekea kila siku  miaka inapungua NI DHAMBI TU, maana tukiwasoma wazazi wetu wa kwanza, pale Mungu alipowaumba  Kusudi kuu la Mungu lilikuwa ni kuishi milele na wala Mungu hakuwawekea mda  wa kuishi kwamba waishi miaka mingapi , jambo hili la miaka lilianza baada ya WAO KUASI KWA KWENDA KINYUME NA MAAGIZO YA MUNGU, hapo ndipo mda wa watu kuishi ukaanza, ndiyo maana ukisoma maandiko jinsi maovu yalivyo kuwa yanaongezeka ndivyo miaka ilipungua

Kwa hiyo usielekeze sana mawazo yako katika kuzingatia mambo ya chakula au  hali ya hewa kuwa hayo ndiyo chanzo cha wewe kuishi miaka mingi, hapo unajidanganya
Kitu pekee cha kukufanya uishi miaka mingi ni wewe kuishi maisha ya kumpendeza Mungu,. kuacha uovu na kutenda mema, hapo ndipo tutapokea maisha marefu na si ya hapa tu bali na ya umilele Mbingu mpya na nchi mpya.

mithali 10:4
4 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. ”

Zaburi 34
12  Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, Apendaye siku nyingi apate kuona mema?
13  Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila.
14  Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT