Baradhuli ni watu gani?

  Maswali ya Biblia

Kibiblia baradhuli ni mtu anayefanya jambo na anajua kabisa si sawa mbele za Mungu, mtu  kama huyo anafananishwa  mpumbavu mtu asiyefaa, anayevuka mipaka.

Watu hawa hutawatambua Kwa tabia hizi, kulingana na maandiko

   WATU WANAOMWAGA DAMU ISIYO NA HATIA
Watu kama hawa ni mabaradhuli Kwa sababu anafanya jambo ambalo anajua kabisa mbele za Mungu ni chukizo lakini yeye anatenda, Kwa. sababu ya tamaa zake Kwa kushindwa kujizuia
mfano tunaweza kuona habari katika biblia Kwa mtoto wa Gideoni, baada ya gedioni kufa, Kuna mtoto mmoja katika ya watoto wake, alimua kuwaua ndugu zake, ili yeye ndiyo awe mwamuzi, Kwa hiyo aliijiri watu ili wawaue ndugu zake, ukisoma maandiko yanasema. watu hao wakuwa mabaradhuli

Waamuzi 9

3 Hao ndugu za mama yake wakanena habari zake masikioni mwa hao watu wote wa Shekemu maneno hayo yote; na mioyo yao ikaelekea kumwandama Abimeleki; kwa kuwa walisema, Huyu ni ndugu yetu.
4 Wakampa vipande vya fedha sabini vilivyotoka katika nyumba ya Baal-berithi, na kwa fedha hizo Abimeleki akaajiri watu wapuuzi mabaradhuli, wafuatane naye.
5 Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze, hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini Yothamu, mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha.

     WATU WANAOABUDU MIUNGU MINGINE KWA MAKUSUDI 
Kundi hili, huwa linafahamu kabisa kuwa jambo fulani si zuri mbele za Mungu lakini utakuta analitenda tena bila woga kabisa, unakuta anaenda kwa waganga bila aibu, anatambika, analoga wengine, mtu kama huyo anaoneka kavuka mipaka kabisa.

Kumbukumbuku 13:12 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo Bwana, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa,

13 Kumetoka katikati yako MABARADHULI kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;

14 ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako;

15 hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.

Hizo ni baadhi ya tabia za watu kama hao, Jambo la kifahamu na kujiuliza Je na wewe  upo miongoni wa watu wenye tabia kama hizo kulingana na neno la Mungu inasema

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Kama ikiwa na wewe ni miongoni mwa tabia kama hizo acha mapema, maana mbele za Mungu ni mambo ambayo ni machukizo ni harufu mbaya, mwisho wa tabia hizo huwa ni kuangamia, lakini Kwa Mungu ni Upendo wala hapezwi na kifo cha mwenye dhambi ndiyo maana Leo hii umekutana na habari hii njema hili ubadilike, basi usiufanye moyo kuwa mgumu kutii maana neema hii haitadumu siku zote kama Leo ukiipuuzia sauti hii, Kuna siku inakuja hata maneno haya hutayaona kabisa.

Nini ufanye jambo la msingi ni wewe kumwamini Yesu kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako maana hakuna njia nyingine ya wokovu zaidi ya Bwana wetu Yesu  Kristo,
ubarikiwe..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT