YAHU KWENYE MAANDIKO NI NANI?

  Maswali ya Biblia

Tusome…

Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni MIALI YA YAHU”.

Neno YAHU lina maana zaidi ya moja,ni jina lingine la YAHWE” ambalo ndilo “YEHOVA

Kutoka 6:2-3
[2]Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;


[3]nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

Hivyo hayo majina matatu yana maana moja na ni jina moja..

Tukiangalia hapo kwenye wimbo ulio bora biblia inasema  upendo una nguvu kama mauti”… ilimaanisha kuwa kama vile mauti ilivyo na nguvu hata mtu asiweze kuurudia uzima tena ndivyo Upendo wa Mungu kwetu ulivyo mkuu kwamba akitupenda ametupenda kweli kweli, pamoja na machukizo tunayomchukiza yanaweza akachukia ila sio kutuchukia kabisa..

Warumi 8:35-39
[35]Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?


[36]Kama ilivyoandikwa, ya kwamba,
Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa,
Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.


[37]Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.


[38]Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,


[39]wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Anaposema pia na miali yake ni kama miali ya YAHU,ikimaanisha Kwa Mungu kunatoka Upendo lakini pia Wivu,hivi vitu viwili huwezi kuvitenganisha kwa Mungu, UPENDO,WIVU

Hivyo kutokana na Upendo wa Mungu uliotupenda bure, hapendi kuona tunakwenda kuabudu miungu mingine na kuanza kuisujudia hapo sasa ndipo tunamtia Wivu ambao unaweza kutupeleka mautini..

Kutoka 20:3-6
[3]Usiwe na miungu mingine ila mimi.


[4]Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.


[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


[6]nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Hivyo hatuna budi kumpenda YAHU, tumtii Katika Neno lake na kuzidi kujibidiisha kuyafanya mapenzi yake ndivyo anavyopendezwa Mungu Wetu..

Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT