TAFSIRI YA MITHALI  18:18,KURA HUKOMESHA MASHINDANO

Maswali ya Biblia No Comments

Tusome…

Mithali 18:18 Kura hukomesha mashindano;  Hukata maneno ya wakuu.

Upigaji wa kura ni njia iliyotumika kuleta suluhisho la jambo fulani, lililo hata Katika utata, ni njia pia iliyoweza kuchagua, viongozi, wamiliki na wenye mamlaka..

 Wakati mwingine njia hii pia Mungu anairidhia ili kuleta majibu sahihi kulingana na jambo husika, ndo mana tukiangalia mfano wa Yona,kipindi kile anakimbilia Tarshish kwa kusudi la kulikataa kusudi la Mungu, wakiwa ndani ya meli bahari ikachafuka na wale watu wakapiga kura ili kujua sababu ya mambo hayo ni nini,na tunaona kura ikamwangukia Yona…

Tunaliona pia jambo hili kwa Mitume,baada ya kuomba kuhusu mrithi atakayerithi sehemu ya Yuda iskariote aliyejinyonga, kwa vijana wale wawili, wakapiga kura,na ikamwangukia Mathiya na Mungu akalichagua hilo (Matendo 1:15-19),

Pia tukiangalia kipindi cha wana wa Israel,mpaka ugawanyi wa ardhi unakamilika ulifanyika kwa kupiga kura,soma  (Hesabu 26:55).

Kupiga kura ilikuwa ni njia bora yenye kuleta majibu yasiyokuwa na upendeleo wowote,au yenye kutegemea upande fulani ,kulalamika kwingi kuliisha kwasababu maamuzi hayakuamuliwa na mtu bali kura ilileta majibu..

Kwa wakati wa sasa pia njia inayotumika kuchagua viongozi ni hii ya kupiga kura ijapokuwa si Katika hali ya kurusha shilingi bali ni maoni ya kila mmoja yanakusanywa na kuhesabiwa na yule aliyezidi hupewa nafasi hivyo kunakuwa hakuna malalamiko…

Hii pia inatuonyesha kwamba Mungu anauwezo wa kuingilia kura zinazopigwa na kuleta majibu yaliyo sahihi endapo tukumshirikisha Katika Maombi na kuzidi kuwa waaminifu Katika Neno lake..

Bwana akubariki…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *