INJILI NI NINI?

  Maswali ya Biblia

Neno injili limetoka na neno la kigiriki euaggelion lenye maana ya “HABARI NJEMA” Kwahiyo maana kuu ya Injili kibiblia ni Habari njema za Yesu Kristo
neno la Mungu linasema

Luka 2:8 “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.

9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.

10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;

11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana“.

Tutatambuaje kuwa Injili inayo hubiriwa ni ya kweli?
Kulingana na neno la Mungu, Injili yeyote au habari yoyote itakayo hubiriwa nje na Bwana wetu Yesu Kristo hiyo si Injili ya kweli, maana katika injili lazima habari yoyote inamzungumze Bwana Yesu, kuhusu maisha ya Yesu, kuzaliwa kwake, kufa kwake, na kurudi kwake mara ya pili hiyo ndiyo injili ya kweli.

Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Lakini ikiwa tofauti na hapo, Moja Kwa moja habari hizo zatoka Kwa yule mwovu, na habari zake huyu mwovu huwa hamzungumziii kabisa Bwana Yesu, zaidi huzungumzia mambo ya mwilini tu, mambo ya ulimwengu huu, kwa kuwatumainisha watu kupenda pesa, hafundishi utakaso, wala kuishi maisha matakatifu, zaidi atawaambia watu MUNGU ATAZAMI MWILI BALI ROHO, unakuta watu wanaishi watakavyo tu.. Sasa hiyo si Injili ya kweli ni YA UONGO Endapo ukiisikia kimbia haraka na utafute uponyaji wa Roho yako kwa kutafuta injili ya kweli ipo wapi, maana ukikosa hiyo jua umepoteza ahadi ulizowekewa na Mungu

Na sasa hivi takribani ulimwengu mzima, Injili habari njema ya Yesu Kristo imeshahubiri, linatulimia lile andiko linalosema “na habari njema zitahubiriwa katika ulimwengu hapo ndipo ule mwisho utakuja”
hii ikitupa angalizo endapo kama utakuwa mpaka hivi Leo hujaitii injili ya Kristo iletayo wakovu, basi wakati wake umekaribia kuisha yaaani neema ya upatanisho Kwa Mungu wetu kuna wakati itaisha na ikiisha kinachofuta ni hukumu tu, Kila mtu kulipwa sawa sawa na alichokitenda, ikiwa ulishindwa kuuchukua msalaba wako na kumfuta Kristo Kwa sababu ya tamaa ya ulimwengu huu mwisho wake ni hukumu,

Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.

Nakupa shauri Leo Itii Injili ili uwe salama, maana Injili pekee ndiyo iletayo wokovu.

Matendo 3:26
“Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake. ”

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT