IFahamu Maana ya Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”.

Biblia kwa kina No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Hekima iliyokuwa ndani ya Sulemani ilikuwa ikumuongoza katika kupambanua ama kufahamu mambo mengi sana, ambayo pia kwetu yanafanyika kuwa ni msaada mkubwa sana kama tukiyasoma na kuyaelewa na kuamua kuchukua hatua.!

Hivyo upo uhusiano mkubwa kati ya Uvivu na umasikini, maaana umasikini hauwezi kuja pasipokuwezeshwa na uvivu!!, Tengeneza mtu hana Fedha halafu asitoke kutafuta aendelee kulala kwa kuukubalia mwili jinsi unavyotaka bila Shaka huyo mtu hatapata kitu!,

Sasa ukisoma hapo anasema “Uvivu humpelekea mtu katika usingizi mzito ” kumbe si usingizi tu lakini ni usingizi mzito maana yake si wa kawaida!.

Kwa nini inakuwa hivyo?, nikwasababu mwili unakuwa idle (haujishughulishi na chochote) hii inapelekea mwili kukaa katika hali ya Uvivu na mwisho wa siku usingizi taratibu utaanza kumchukua huyo mtu!.

Hivyo mwili utajenga tabia siku baada ya siku na mwisho kabisa umasikini utaingia kwa kiasi kikubwa!!.

Sasa mstari huu uko unalenga kitufundisha katika sehemu kuu mbili ambazo tutakwenda kuzitazama, unalenga katika uvivu wa mwili lakini pia Uvivu wa rohoni.

UVIVU WA MWILINI.

Mungu alivyotuumba alikusudia tufanye pia kazi sio tukae tu pasipo kujishugulisha na chochote. Na ndio maana utaona hata Adamu alipewa jukumu la kuitunza ile bustani ya Edeni sio kwamba Mungu asingeliweza kuitunza pia, angeliweza lakini hakutaka kufanya hivyo akampa jukumu hilo Adamu. Kuonyesha Mungu pia kakusudia tufanye kazi (ikiwemo na sisi Watakatifu).

Kama Mtume Paulo alivyowaambia katika kanisa Thesalonike wajishugulishe pia na kazi ili wapate pia chakuwagawia na wengine
2 Wathesalonike 3:10″
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. ”

Soma pia 1 Wathesalonike 4:11.

UVIVU WA ROHONI.

Kama jinsi ilivyo katika Mwili na ndio ilivyo katika roho, kama Mtakatifu ni mvivu wa kusoma Neno anafunua biblia Jumapili kwa Jumapili,haombi wala kukesha yeye muda huo wa kuomba na kusoma Neno anautumia katika kuangalia Tamthilia,kucheza Magame, kukaa katika mabaraza ya watu wenye mizaha,uvivu katika kushuhudia wengine waokoke, huyu mtu atadumaa katika roho(Spiritual domanant) atakuwa ni Mkristo asiekuwa na matunda.

Hivyo uvivu katika pande zote mbili una madhara hivyo tuuepuke tujizoeze kusoma Neno, lakini pia kufanya kazi za Mikono na kumtumikia Kristo kwa nguvu zote tusiruhusu hali hii ituvae.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *