Mithali 25:23
[23]Upepo wa kusi huleta mvua;
Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
Biblia imezungumzia jinsi upepo wa kusi unavyoweza kuleta mvua, na hasemi upepo huleta mvua, bali “upepo wa kusi” akimaanisha kila aina ya upepo ina tabia yake ya kipekee,mfano wa upepo wa kaskazi unaleta joto,na aina nyingine za pepo zina tabia zake…
Hii inatufundisha nini?
Hata sisi wanadamu tunauwezo wa kuvumisha pepo, na pepo yetu hii inajulikana kama UVUMI, uvumi ni taarifa ya Jambo Fulani ambazo husambazwa kwa vinywa vyetu wenyewe, jambo lolote unalolitoa kwenda sehemu,kwa jamii au watu fulani,uwo ndo upepo,unatakiwa kuwa nao makini sana mana usipozingatia unaweza ukaleta madhara au faida…
Na ndo mana kipengele kinachofuata anasema asingiziaye huleta uso wa ghadhabu, akimaanisha kusingizia ni sawa na usengenyenyaji, mtu anayechukua taarifa zisizo Katika ukweli na kizipeleka kwa mwingine mwisho wake ni kuchukiwa au kusababishiwa madhara kwa wale waliotolewa taarifa zao, kwasababu ni uvumi,na kila uvumi una matokea yake..
Lakini tukiwa watu wa kupeleka habari njema za Yesu Kristo, kuhubiri na kushuhudia basi tufahamu ni upepo wa heri tunauvumisha kwa watu, basi tufahamu mema mengi yatatupata badala ya ghadhabu na tutapendwa badala ya kuchukiwa..
1 Petro 2:1[1]Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
Jiepushe na dhambi ya usengenyenyaji,kuwazungumzia wengine vibaya
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.