Maana ya Mithali 1:17 mtego hutegwa bure mbele ya macho ya ndege yeyote

  Maswali ya Biblia

Shalom,

Yapo mambo mengi Mwanadamu amekuwa akijiuliza kuhusiana na Mungu lakini mwisho wake ni kutokupata majibu Katika ukamilifu wote, mfano unajiuliza ikiwa Mungu anafahamu jambo ambalo litakwenda kutokea mbele yako na pengine litakusababishia madhara makubwa kwanini asiingilie kati na kunizuia badala yake ananiacha na kudhurika mwisho wake najikuta naenda kuzimu, ni kama Mungu anaonekana hana Upendo? Ikiwa na wewe ni muhanga mmojawapo wa Maswali hayo, tutafakari hapa..

Maandiko yanasema..

“Kwa kuwa mtego hutegwa BURE, Mbele ya macho ya ndege ye yote”.( Mithali 1:17).

Tutafakari mfano wa mtu anayaweka mtego wa ndege kwa ajili ya kutega kitoweo chake, ivi unafikiri Mungu hampendi ndege yule, au Mungu hakumpa ufahamu wa kujiepusha na maadui zake..

Mfano wa mtu avuaye samaki,je pia hao Mungu awapendi samaki wake aliowaumba..

Kitu chochote mpaka inafikia sehemu kinatafutiwa njia mbadala ili kipatikane fahamu kitu hicho kimeshindikana kukamatika kirahisi hivyo kimetafutiwa njia  nyingine, si kazi rahisi kumkata ndege aliyekaribu yako kwa mikono,haiwekzekani,au panya kumkimbiza ili umshike kwa mikono yako, ni Jambo gumu kidogo, si rahisi..

Sawa na samaki awe Katika mazingira ya kuelea ndani ya Maji na utake kwenda kumvua kwa mikono, laweza kuwa jambo gumu, kwasababu ndani yao tayari Mungu alishawawekea jinsi ya kujitoa kwa maadui zao,wamepewa kuelewa maadui zao hawana wepesi na uhodari ambao wanao wao, haijalishi ni vingi vipi tutawavutia wanavyovipenda..

Pia kwa wanadamu Mungu ameshatupa na kutuwekea uwezo mkubwa sana ndani yetu wa kumshinda adui yetu shetani,Na shetani analijua hilo kwamba hawezi kuja kutushika na kutukamata hivi hivi, hana uwezo huo, anafahamu kabisa hawezi kutupata, lakini mbinu anayotumia ni kujiundia mitego mbalimbali itakayokunasa, na akishakunasa anakuwa na uwezo wowote hata kukuondoa duniani..

Na mtego mkubwa shetani anaotumia kuwanasa watu ni Uasherati, anao uwezo wa kukuletea mwanamke kahaba ili uingie kwenye uzinzi, na baada ya hapo lengo lake ni ili ukosane na Mungu wako ili ayaachilie mapepo yake upate magonjwa ufe kabla ya wakati wako..

Hayo yote hawezi kuja kuyaleta  hivi hivi ,mpaka akuekee mtego, na ndo hapo unakuletea mwanamke kahaba mzuri, limama lenye pesa anakulaghai na bila kufikiri ni mtego wa shetani unakwenda kuuvaa, ukifikiri Mungu atakuepusha nao, Mungu hawezi kufanya hayo kabisa..

Pitia kitabu cha mithali sura ya saba 7 yote uone kijana aliyekatika upumbavu akitegwa na mwanamke kahaba na mwisho wake jinsi ulivyo..

Mithali 7:21-27[21]Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.

[22]Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;

[23]Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.

[24]Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.

[25]Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.

[26]Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.

[27]Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba

vya mauti.

Ndege aliyenaswa Katika mtego ametaka mwenyewe si kwa udhaifu alionao,tamaa ndizo zilizomponza..Unapoingia kwenye shida na matatizo Fulani na unafahamu kabisa ni dhambi iliyokufanya mpaka yakakupata hayo, hivyo usianze kunung’unika na kumlaumu Mungu kwamba akukuweka nayo mbali hapo kabla, kumbuka Mungu alishaweka na kukupa huo uwezo tokea zamani, na hata shetani akiulizwa analo atakalojitetea, atasema yeye aliweka mtego wake hakumuita mtu wala kumlazimisha,alichokiweka kwenye mtego wake alikifata mwenyewe nikamnasa,nikamwangamiza kwa tamaa yake..

Biblia inasema..

Hosea 4: 6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”

Tukiyakosa maarifa ya kufahamu hila na njama zake, na kuelewa mafumbo yake tutajikuta tupo kwenye Matatizo makubwa ambayo mwisho wake tutashngaa tumefikaje hapa..

Ufunuo wa Yohana 2:24-25

[24]Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.

[25]Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.

Tuna wajibu wa kila mmoja wetu kuzijua mitego ya shetani, na kupata maarifa zaidi jinsi gani yakuweza kujilinda na hila zake na tunaifahamu kwa KUSOMA Neno la Mungu,huko tutapata kujua siri zote na mambo yote ya uwongo wa shetani, na ndo mana anapiga vita watu wasiwe wasomaji wa biblia,..

Kuwa mtu wa kupenda kusoma sana biblia, usiwe msomaji tu kama kitabu cha Hadithi,bali kuwa mtu wa kutafakari na kumruhusu Mungu akufunulie mambo mengi,kwa kuwa hiyo ndo nuru yetu…kwasababu mitego ya adui ni mingi na vishawishi pia, uwezo Mungu ametupa hivyo tuongeze maarifa kwa kusoma BIBLIA SANA

Jaribu au mtego wowote hakuna ambao haukuandikwa Katika biblia na jinsi gani ya kuweza kuushinda, kila kitu kimo hukohuko kwenye maandiko, weka desturi yako ya kusoma biblia ili usiwe na sababu ya kupeleka malaumu Mbele za Mungu..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT