Bwana Yesu asifiwe Karibu tena katika kujifunza neno la Mungu litupalo uzima wa milele
Hapo maandiko yaliposema
Warumi 3:22 “ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;”
Hapa tuzingatie mambo haya hili tuelewe maana halisi ya mstari huu, ukisoma hapo maandiko yanasema “wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu” sentensi hii ilimaanisha kuwa, Jambo ambalo limeshatendeka zamani, yaani jambo lililokwisha kutendeka, na ingekuwa linaemdelea kufanyika maandiko yangesema kwa kuwa wote wanafanya dhambi, lakini maandiko yanasema WAMEFANYA DHAMBI
Na dhambi yenyewe si nyingine zaidi ya wazazi wetu wa kwanza Adam na Hawa
Warumi 5:19 “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki”.
Kwahiyo dhambi ya wazazi wetu wa kwanza ndiyo iliyotufanya tuonekane kuwa tumetenda dhambi,na kwanini ilionekena hivyo ni k wa sababu sisi tulikuwa katika viuno vya wazazi wakati walipokuwa wanaemda kinyume na agizo la Mungu, ndiyo maana hata hivi leo tunaona mtoto anapozaliwa anapokuwa katika umri ambao haelewi chochote lakini vitabia anaweza vionyesha hadi ukashangaa nani kamfundisha.
Mfano labda ulimpa kitu kisha badae ukamuomba, lakini akakunyima kabisa, sasa kwa tabia hiyo aliyoionesha ya uchoyo ukiangalia bado ni mdogo hajui chochote sasa kwanini ni kaonysha tabia ya uchoyo hii moja kwa moja inatupa uhakika kuwa sisi sote tumefanya dhambi. Yaani kila mwanadamu anayezaliwa anakuwa na asili ya dhambi ndani yake
Lakini japo tuna asili ya dhambi lakini Mungu alitupa njia ya kuondoka asili hii, na njia yenyewe si nyingine zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo, yeye pekee ndiyo anayeweza kutuondolea asili yote ya dhambi ambayo tumeipata kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza, Na tunaitoaje asili hii
Tusome
1 Yohana 1:8 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”.
Pale tunapomwamini Yesu Kristo maishani mwetu na kuonyesha toba ya kweli, kwa kuziungama dhambi zetu hapo hapo dhambi huondolewa lakini ikiwa tofauti na hapo hakuna hondoleo la dhambi, kwa sababu Yesu pekee ndiyo aliyebeba mashtaka yote ili sisi tuwe huru na kuondokana katika utumwa wa dhambi, kwa sababu dhambi haindolewi kwa kushika sheria sana lah! Bali ni kwa Yesu pekee
1Yohana 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu”
Hakuna njia tofauti na Bwana wetu Yesu Kristo ikiwa leo utashindwa kumpokea ili awe Bwana na mwokozi wa maisha yako bado utaendelea kuwa mtumwa wa dhambi tu (warumi 10:9-10 ) lakini kama leo ukichukua hatua mapema maandiko yanasema utakuwa huru kweli kweli
Kwa sababu ya kale yanapita na unakuwa kiumbe kipya
2Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”.
Je umeokoka, ikiwa bado fanya uwamuzi leo ili uwe salama, na kisha baada ya hapo tafuta kanisa la kiroho, ili uweze kubatizwa ubatizo kulingana na neno la Mungu wa maji na kwa jina la Yesu na baada ya hapo zidi kudumu katika fundisho ili Mungu azidi kukukamilisha
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.