DHABIHU NI NINI?

  Maswali ya Biblia

Katika agano la kale dhabihu ni Aina ya sadaka zilizotolewa Kwa Bwana zikihusisha vifo vya wanyama. Kwa jina lingine tunaweza kuita KAFARA.

Bwana alisogezewa wanyama kutoka katika makundi ya wanyama safi/ wasio najisi Kama ng’ombe, mbuzi na kondoo. Walichinjwa kama sadaka wakachomwa madhabahuni na damu kunyunyizwa ili kuleta upatanisho kwaajili ya dhambi za watoa dhabihu

Tofauti na dhabihu, zilikuwepo sadaka za unga, amani, malimbuko n.k
Sadaka hizi tunaona zilitotewa na watu wa agano la kale

Je na sisi wa agano jipya Je tunatakiwa kumtolea Bwana dhabihu za wanyama?

Jibu ni Hapana! Katika Agano jipya hatuhitaji tena kumchinjia Bwana wanyama ili tupate rehema au neema zake.

Tutatazama Jambo ambalo kwa sisi wa agano jipya, tunaweza kupokea msamaha wa dhambi zetu, pasipo damu ya wanyama, nayo ni..

  • Ni Kwa kupitia dhabihu ya mwanakondoo Yesu Kristo iliyotolewa kwaajili ya dhambi za ulimwengu mzima. Kwa damu yake iliyomwagika msalabani tunapatanishwa na Mungu.
    Na tena tangu dhabihu hii itolewe, Bwana amezikataa kabisa zile za wanyama ambazo alizikubali hapo mwanzo

Waebrania 10:3-10

Hivyo Sisi kama WaKristo hatuna ruhusa tena ya kumwaga damu ya Mnyama Kwa Lengo la kutafuta majibu ya maombi yetu Kwa Mungu.

Lakini kwa jinsi mambo yalivyo, Kristo akiwa ni njia, kiongozi, mwalimu wetu mkuu na mzaliwa wa Kwanza katika mambo yote.
Alijitoa sadaka kwaajili yetu, akiyatimiza mapenzi ya Baba yake.
Na Sisi tukiwa kama wafuasi wake tunapswa tujitoe sadaka.

Warumi 12:1
[1]Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

  • Yaani asema, Kwa Bwana ibada yenye maana kwake, ni sisi kuitoa miili yetu kuwa kafara hai

Namna gani?

Kwa kujitoa Kwa Bwana kuyaishi mapenzi yake, Kwa kuzikana tamaa za miili yetu na kulifata kusudio lake, Kuishi maisha matakatifu ambayo ni changamoto kubwa Kwa wengi kuyaishi.
Na ndicho anachotaka Bwana toka kwetu, tumtii Yeye, tuuache ulimwengu na mambo yake tumfuate yeye.

Je umeokoka ikiwa bado, basi fanya maamuzi Leo mpokee Yesu Kristo awe patanisho lako la Milele..

NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa msaada zaidi
Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312

LEAVE A COMMENT