Elewa maana ya neno kuapiza kama linavyosomeka katika Mathayo 5:21-22

Maswali ya Biblia No Comments

Mathayo 5:21  Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

22  Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto

Hapo tunaona Bwana anatupa uelewa mwingine wa Kuhusiana na dhambi ya kuua, kwasababu tokea hapo mwanzo ilidhaniwa kuua ni kitendo cha kumpiga au kumchinja nduguyo mpaka kufa kama kaini alivyofanya kwa nduguye habili, ukifanya hivyo imekufanya kuwa muuaji,

Lakini Bwana anasema.. jambo tu la kumuonea hasira ndugu yako,au kumfyolea na kumwapiza hapo tayari wewe ni muuaji..una kosa la kuua…

Tuelewe maana ya haya maneno, hasira,kufyolea,kuapiza..

Unapoonyesha hasira kwa ndugu,ndiyo inayopelekea vinyongo, wivu na uchungu moyoni, kwa mtu mwenye vitu hivi mbele za Mungu anaonekana hastahili..

Kumfyolea ndugu yako ni kitendo cha kumwita jina lisilofaa,kama mpumbavu wewe,mjinga, ukimaanisha ni mtu asiye kuwa na akili, ni kosa, pia Maaandiko yanasema unastahili uketishwe kwenye baraza utolee hesabu yake..

Kumwapiza ni jambo baya sana Kwasababu hili limeenda mbali kwa kudiriki kumtamkia Maneno yasiyofaa au yenye laana ukimuonyesha kama ni mtu mwovu, yapo maneno ambayo hayastahili kabisa kumuita ndugu yako, kama mwana haramu, au “shoga wewe” , Pepo wewe, n.k, na maneno mengine ambayo hayana uzuri wowote,ni matusi tu, sasa huko ndiko kumwapiza..

Adhabu ya makosa haya ni sawa na kutupwa Katika ziwa la moto, ndivyo Yesu Kristo anaifananisha..

Tusiwe na fikra kwamba kufanya mauaji ni mpaka tuue,au umwage damu, hayo yanaweza kufanyika Katika mioyo yetu na midomo yetu kabla ya tendo lenyewe la kuua..

Tukijazwa Roho Mtakatifu tunaweza kuzishinda hizi tabia zinazotoka katika miili yetu..

Zamani za agano la kale ilikuwa  si kitendo cha kumpiga mzazi wako, Hapana, bali kumwapiza tu adhabu yake ilikuwa ni hiyo hiyo kifo..Ilionekana ni kosa moja tu..

Kutoka 21:17 “Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa”

Mkabidhi leo Yesu Kristo Maisha yako, muda tulio nao ni mchache sana, sababu kubwa ya yeye kufa msalabani ni ili uwe na uzima wa milele,usiingie Katika moto usiozimika..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *