ELEWA UKINA WA MITHALI 21:17 Mtu apendaye Anasa atakuwa MASKINI

  Maswali ya Biblia

Bwana Yesu kristo Asifiwe. Karibu tujifunze Biblia

SWALI : Ni Nini maana ya Mithali 21:17 ” Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri”
JE mstari huu una maanisha Nini?

JIBU : Kwanza yatupasa kufahamu mstari huo una maana mbili,
Ya kwanza ni ya kimwili ikimaanisha ” Watu wapendao Anasa hatma zao ni kutofanikiwa” sababu hata kile kidogo kinachopatikana hakizalishi zaidi Wala kuwekwa akiba zaidi ya starehe Yaani pombe, wanawake, vitu vya bei ghali ili waonekane wa kisasa n.k

Maandiko yanaposema apendaye mvinyo na mafuta, hayo ni “marashi ya gharama kubwa” Ambayo hapo zamani walinunua matajiri. Kwa mfano mtu ana kipato Cha laki mbili kwa mwezi anakwenda kununua marashi ya laki moja! Ili tu aonekane wa kisasa, Sasa Anasa kama hizo mwisho wake ni ” Umaskini”.

Majivuno, na kukosa Adabu hayo ni matunda ya Anasa, hivyo Maandiko yanatuonya kuwa Anasa ni adui wa mafanikio .

Kiroho pia Anasa ni tunda la ufukara wa kiMungu. Mtu wa Anasa hutumia muda isivyopasa mfano, atatumia mda wake wa ziada kufanya starehe za kimwili, na Wala si mambo ya Rohoni

Na Bwana anasema..

Luka 8:14
“Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.”

Hapa Tunaona kuwa Anasa huizonga mbegu ya Mungu ndani ya mtu.

Tukija katika maisha ya Sasa anasa hizo ni kama kukaa kwenye tv Kila kukicha, series za kidunia, kushinda mitandaoni kufatilia udaku tu, kuchat mambo yasiyo ya kiMungu na hao maboyfriend na ma girlfriend, kushiriki sherehe sherehe za kianasa na zisizokuwa na mipangilio kuwaza mambo ya kidunia ikiwemo “ku-party weekend”, na mambo mengine kama hayo yanayokupa Raha za kimwili na kihisia lakini hukubomoa Rohoni.
Unapoteza wakati kufanya hayo badala ya kusoma neno na kuomba, kama yasemavyo Maandiko

Sasa kama wewe unajiita ni MTU uliyeokoka, na unaishi maisha kama hayo usitazamie kumzalia Mungu matunda, Utakuwa ni yule yule milele, Na pia biblia inatuambia ni heri kuona kwa macho kuliko kutanga-tanga kwa tamaaa(Mhubiri 6:9)
Mpendwa si  kila taarifa uzipate, Kila kitu ufatilie, Kila kitu utende wewe, Viache vingine vikupite ili upate muda wa kuwa karibu na Bwana MUNGU wako. KOMBOA WAKATI

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT