Ikiwa tunaokolewa kwa Neema, kwanini wokovu tuupate kwa nguvu..

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU, Tufahamu kabisa mchango wetu Katika Neema ya Wokovu haupo

Tusome..

Waefeso 2:8-9[8]Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

[9]wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu…

Sasa ikiwa ni hivyo, kwanini biblia iseme tena hivi

Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.


Tukumbuke kuwa mshitaki wetu ibilisi ambaye ni adui yetu mkubwa, yeye ndiye anayeleta ugumu katika maisha yetu ya wokovu. Na hivyo inahitajika nguvu ya kumshinda ili tuweze kuiona na kuiendea njia ya wokovu vizuri, njia ni nyembamba na zaidi sana imesonga…

Mathayo 7:13-14[13]Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

[14]Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.


Kwa mfano, mtu anaweza kupata kikwazo kutoka kwa shetani akashindwa kuhudhuria ibaada pengine wazazi wakamzuia, kazi zikawa nyingi na wakati mwingine mazingira yakawa si rafiki kwake, sasa mambo kama haya ukiyaruhusu unafikiri ni rahisi kuurithi ufalme wa mbinguni? Hapana itakulazimu utumie nguvu kulazimisha mambo kama hayo, kubali kupoteza vingine kwa ajili ya wokovu, kubali hata kuchukiwa mradi tu upate ufalme wa Mungu. Na hiyo ndiyo maana ya kusema ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu tu ndio hufanikiwa kuuteka

Yesu alituambia tuombe ili tusiingie majaribuni, (Mathayo 26:41)
Shetani anatuwinda kila saa tena ukiwa huombi kwa ajili ya kulinda wokovu uliopata bure bila kuusumbukia,,utapitia shida tu, ni mvivu jua kwamba adui yetu yeye anakesha kwa ajili ya kutuwinda, na ipo siku atakujaribu kama alivyofanya kwa akina Petro hadi wakamsaliti Bwana Yesu. Waliambiwa wakeshe lakini hawakuzingatia walichoambiwa wakalala na matokeo yake yakawa mabaya.

Hata sisi tusiposimama katika maombi, tusipojitaabisha kwa kufunga au kutomtumikia Bwana Yesu itakuwa vigumu kuutunza wokovu wetu na tunaweza hata kuupoteza.


Kumwamini Yesu peke yake haitoshi lazima tupambane tutumie nguvu kupigana vita ili tumshinde shetani na kuutunza wokovu wetu kika siku.


Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *