Nini maana ya huu mstari,huwapatiliza wana maovu ya baba zao.(Kutoka 20:5-6)

  Maswali ya Biblia

Shalom, karibu tujifunze Maneno ya Uzima..

JIBU..Tusome

Kutoka 20:5-6[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

[6]nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Tukiangalia katika mstari wa 5 neno linasema ‘hata kizazi cha tatu na cha nne cha’ WANICHUKIAO’ kwa hiyo si kwamba Mungu huwapatiliza wote ila ni wale wanaomchukia, yaani ikiwa baba anaabudu sanamu na mtoto nae akafanya vilevile baba anavyofanya basi laana itatoka kwa baba kwenda kwa mtoto…


Wakati ule wana wa Israeli walichukuliwa kwenda utumwani huko Babeli na Ashuru kwa sababu hawakumpenda Mungu, wao waliabudu miungu mingine ambayo baba zao na wafalme wao waliiabudu, walitakiwa kutubu lakini wao waliendelea na uovu huohuo.

Tukiendelea mstari wa 6 unasema ‘NAMI NAWAREHEMU MAELFU ELFU WANIPENDAO NA KUZISHIKA AMRI ZANGU’ maana yake ni kwamba, ikiwa wazazi wamefanya uovu mbele za Mungu, na laana ya Mungu ikawa juu yao lakini watoto wao wakampenda Mungu basi ile laana haitawapata…Watoto watendao haki ya Mungu watapata rehema watakuwa tofauti na baba zao kama vile hawakuzaliwa katika familia yenye uovu.

Tunaliona hapa…

Ezekieli 18: 20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake”.


Bwana akubariki,

Nguvu ya Roho Mtakatifu ikusaidie kuifuata njia ya Mungu ili kuepuka kubeba laana za wazazi…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT