FAHAMU MAANA YA HUU MSTARI,

  Maswali ya Biblia

Wakorintho 3:17 “Basi ‘Bwana’ ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru”

JIBU:

Maana ya Kauli hiyo kwa tafsiri nyingine ni kuwa , kama Roho wa Mungu hayupo basi mahali hapo panakuwa hakuna uhuru wowote, kwa mujibu wa maandiko katika biblia.

Lakini inapaswa tunafahamu ya kuwa ni aina gani ya uhuru Roho Mtakatifu analeta.

Katika biblia tunachopaswa kujua ni kuwa Roho Mtakatifu alikuja kuleta Uhuru wa aina mbili.

Uhuru wa kututoa katika utumwa wa maisha dhambi na mateso.

Uhuru wa kututoa katika utumwa wa sheria.

Tuanze na uhuru wa kututoa katika utumwa wa maisha ya dhambi pamoja na mateso.

Tunaona katika siku ile Bwana wetu Yesu alipoanza safari ya huduma yake katika kuhubiri injili alisema maneno haya.

Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa

19 na kutangaza mwaka wa Bwana aliokubalika.

Maandiko yanatuonyesha kuwa Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya watu wake kazi kubwa ilikuwa ni ya kuwatoa watu katika vifungo vyao mbalimbali ambavyo walikuwa navyo kutokana na dhambi na mateso ya ibilisi, yaani waliokuwa wanasumbuliwa na mapepo, waliokuwa wanateswa na magonjwa, na hofu, na mauti, na shida hayo yote yalikuja kuondolewa na Roho Mtakatifu mwenyewe,

Na ndio maana ukizidi kusoma tena katika Isaya 61:3-4 utaona unabii huo wa Roho Mtakatifu unaendelea kusema…

Isaya 61:3-4[3]kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.

[4]Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.

Pia Unaona Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kuwatoa watu katika huzuni zao, kuwafariji,kuwapa mataji ya utukufu na sifa. Uhuru wa namna hii ni uhuru ambao hakuna mwanadamu awaye yeyote hapa duniani angeweza kuutoa kwa mwanadamu mwingine zaidi ya Roho wa Mungu mwenyewe..

Na pia alikuja kutuokoa sisi tuliokuwa tunaishi chini ya sheria, tukombolewe katika laana ya sheria.

Wagalatia 4:3-7[3]Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

[4]Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,

[5]kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.

[6]Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.

[7]Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.

Kwa kawaida, huwezi kwenda kuupeleka mkono wako mwenyewe katika tundu la nyoka akung’ate kila wakati, kisa tu dawa ya kutibu sumu ipo, hapana, tofauti na hapo utakuwa kama mwendawazimu, bali utachukua tahadhari kubwa sana, kwa kujitahidi kukaa mbali na nyoka, kwasababu unatambua kuwa sumu yake nyoka ikingia katika mwili wako inakupelekea kupata madhara isipotibiwa mapema na hivyo kupelekea Kifo au madhara makubwa..

Vivyo hivyo na sisi maadamu tumeshahesabiwa haki katika Yesu kristo kwa kumwamini, ni jukumu letu sote kama wana wa Mungu tukae mbali na dhambi, kwa kadiri tuwezavyo,na tujitahidi kuishi maisha matakatifu ili tupate kumzalia Mungu matunda na hiyo ndio ishara ya kuamini kwetu.

Hivyo kwa hitimisho yatupasa kutambua ya kuwa Roho Mtakatifu ametuletea uhuru mkubwa sana hapa duniani. kiasi kwamba mtu awaye yeyote atakayempokea, atakuwa amewekwa HURU KWELI KWELI.

Jambo ambalo wengi wetu hatulifahamu, tukidhania kuwa kukaa kwa Mungu ni kuwa mtumwa, sivyo anza kuziondoa hizo fikra

Jambo kuu unalopaswa kujiuliza je umeshampokea Roho Mtakatifu ndani yako,

Kama jibu ni la, unasubiri nini? Kumbuka Pasipo Roho Mtakatifu huwezi kwenda katika unyakuo, na haji ndani yako isipokuwa kwanza umemwamini Yesu Kristo, kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa na kuwa tayari kuyaacha mambo yako maovu uliyokuwa unayafanya huko nyuma na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele, na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38 hivi vyote vinaenda sambamba…

Na hapo ndipo Mungu atakapokupa kipawa cha Roho Mtakatifu ndani yako bure kabisa..

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT