Fahamu maana ya kibiblia ya sulubisha?

  Maswali ya Biblia

Neno hili sulubu ndilo hutoa maana ya neno sulubisha au sulibisha..

Na maana halisi ya sulubisha ni kuadhibu kwa kuning’iniza kwenye msalaba au mti,nguzo ndefu iliyonyooka kwa kufungiwa hapo au kugongelewa na misumari miguuni na mikononi na huachwa hapo hapo kwa mateso makali itakayokupelekea Mpaka kifo..

Na  adhabu hizi zilitumika kipindi cha zamani kwenye Ufalme uliokuwa na nguvu yenye ukatili ,mfano wake kama Ufalme wa Rumi

Adhabu hii ilitolewa kwa waliofanya makosa makubwa,ikiwemo uvunjaji wa  amani,uhaini au uuaji,hawa hawakupewa adhabu za kawaida kama kunyongwa au kukatwa kichwa bali walipewa adhabu ya kusulubishwa kwenye msalaba ili apitie mateso makali ya muda mrefu, kwa sababu kitendo cha kuekwa msalabani itakulazima ukae siku nyingi hata wiki mpaka umauti ukukute, kipindi chote hicho unapitia mateso makali sana..

Ndivyo walivyoichangua adhabu hii kwa Mwokozi wa ulimwengu mzima YESU KRISTO, ambaye hakuwa na hatia yoyote wala kosa iliyopelekea kusulubishwa jambo ambalo mtawala pilato alithibitishiwa kwamba Yesu hana uovu wowote (Luka 23:4) Lakini kwa kuwa maandiko yalishamtabiria Kristo, kwamba ni lazima apitie hayo yote ili sisi  tupate kukombolewa, tupate ONDOLEO LA DHAMBI,kwa kifo chake tu pale msalabani..

Kitendo alichokifanya Bwana,ni gharama kubwa sana isiyoweza kulipwa na Mwanadamu yoyote, alisulubiwa uchi bila nguo yoyote, alidhalilishwa sana, alipigwa sana kwa mapigo mengi yote ni ili mimi na wewe,mimi na yule tupate msamaha wa dhambi na maovu yetu na kutuepusha na hukumu itakayojia ulimwengu…oh haleluya,

Maandiko yanasema..

Waebrania 2:3  sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.

Umempokea YESU KRISTO maishani mwako?

Wakati ni huu,Neema bado ipo..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT