Fahamu maana ya Mhubiri 1:9 wala jambo jipya hakuna chini ya jua. 

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mwana wa Mungu,karibu tuyatafakari Maneno ya uzima…

JIBU….

Embu tusome…

Mhubiri 1:2-11
[2]Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.


[3]Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?


[4]Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.


[5]Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.


[6]Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.


[7]Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.


[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.


[9]Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.


[10]Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.


[11]Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.


Ukiangalia hivyo vifungu utaona hakumaanisha uvumbuzi na maendeleo ya kibinadamu maana hayo yalikuwepo tu hata wakati wa Sulemani.. anaendelea kusema..


[29]Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.


Kwa hiyo tunaona kumbe alimaanisha kazi ya Mungu aliyoifanya chini ya jua pamoja na mifumo yote ya kiulimwengu hakuna lolote jipya ambalo limetokea…Mhubiri anasema hata jua lipo vile vile kama Mungu alivyolitengeneza halijabadilika rangi wala chochote na linaendelea na utaratibu wake ule wa siku zote wa kuchomoza na kuzama, hata mambo ya sayansi yakiendelea kwa namna gani hakuna hata siku moja vile alivyoviumba Mungu vikabadilika, mfano upepo utabaki kama uvumavyo, maji yatapita katika mkondo wake hata mwanadamu akijitahidi kwa namna gani bado ataishi vile vile kama watu wa kale, atazaliwa na atakufa.

Na katika mifumo ya kiulimwengu mambo ni yale yale, wameshatokea wafanyabiashara na wataendelea kutokea, walikuwepo wajenzi na wataendelea kuwepo, maudhui ya maisha ni ileile kinachobadilika ni mwonekano tu. Mtu akivaa suti leo kesho akabadilisha akavaa kanzu hiyo haimfanyi yeye kubadilika na kuwa malaika atabaki hivyo hivyo. Hata ngano inatengeneza mandazi leo kesho inatengeneza mikate lakini bado inaitwa ngano hakuna siku itabadilika na kutengeneza ndizi…

Ndugu maandiko yanatuambia nini cha kifanya tuwapo hapa duniani ili kwamba tusipoteze muda mwingi kwa fikra za kuleta jambo jipya hapa duniani. Neno linatufundisha kuishi kwa kumcha Bwana maana kwa njia hiyo tutaleta jambo jipya ndani yetu ambalo ni kurithi uzima wa milele.


Na Mhubiri anamaliza kwa kusema haya


[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *