HII NI TAFSIRI YA Wagalatia 6:1 ” Ukijiangalia Nafsi yako usije ukajaribiwa wewe Mwenyewe”

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Shalom karibu katika kujifunza Maandiko matakatifu

Wagalatia 6:1
“Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.”

JIBU: Hapa Maandiko yanatupa mwongozo Namna sahihi ya kuwarejesha upya wale wapendwa Walioanguka dhambini.

Biblia inatuasa tuwarudishe kwa upole pasipo  kuwakaripia au maneno makali au kuwalaumu.
Mfano unakuta mpendwa amerudi nyuma katika Ulevi aliokuwa nao kabla ya kuokoka. Ndiposa biblia inatuasa kutumia Busara na maneno ya upole kuwarudisha ili iwe rahisi kugeuka na kutubu, Kuliko kutumia ghadhabu au kumkaripia n.k

Tunapotumia kauli za lawama na mashutumu sio rahisi kuwavuta wapendwa hawa na matokeo yake ni kuwafanya wapate hasira badala ya kutubu.

Lakini tunapoangalia sehemu ya pili anasema “.. Ukijiangalia Nafsi yako usije ukajaribiwa wewe Mwenyewe”.

Hii inamaanisha kwamba hata sisi wenyewe tunaweza jaribiwa na shetani tuwapo katika kuwarejeza wengine waliokengeuka na Wokovu
Mfano kama ni mlevi anaweza kukurushia maneno ya kashfa au matusi nawe UKAGHADHABIKA na kuanza kurudisha lugha za matusi kwa hasira uliyo nayo juu yake, Naam huo tayari ni ushindi mkubwa wa dhambi

Baadhi ya watumishi wa Mungu walijaribiwa na kuangukia katika dhambi ya Uzinzi walipokuwa wakifanyia huduma watu wa jinsia tofauti, si hao tu Bali wengi ambao Walinasa katika anasa zao wale walipokuwa Wakiwashuhudia habari za Yesu na hivyo kujikuta majaribuni na hatimaye DHAMBI!

Hivyo imetupasa kuwa makini na kujichunguza nafsi zetu tupelekapo habari njema za Yesu kwa watu WALIOCHANGANYIKA . Kwasababu shetani naye anatuwinda sisi pia hivyo kwa kudumu katika Maombi nakulishika Neno hakika tutajilinda wenyewe dhidi yake, hiyo ndio Maana ya hilo neno katika

Wagalatia 6:1″ Ukijiangalia sana Nafsi yako usije ukajaribiwa wewe Mwenyewe

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT