YULE TAJIRI NAYE AKAFA, AKAZIKWA

Biblia kwa kina No Comments

YULE TAJIRI NAYE AKAFA, AKAZIKWA.

Luka 16:22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. YULE TAJIRI NAYE AKAFA, AKAZIKWA”.

Nilikuwa natafakari kwanini biblia imetumia hayo maneno “AKAFA, AKAZIKWA“, tofauti na yule maskini ambaye alipokufa “AKACHUKULIWA NA MALAIKA.”

Ndugu, fahamu kuwa ukifa na dhambi usifikiri kuwa malaika watakatifu watakuchukua kwa furaha…ukifa unazikwa kaburini (yaani unashuka kuzimu). Ndicho kilichomtokea huyu tajiri ambaye biblia inasema alikuwa anakula siku zote kwa anasa na kupuuzia neema ya wokovu, alipokufa alishuka kuzimu moja kwa moja (ALIZIKWA).

Lakini Lazaro maskini alipokufa hakuzikwa, bali alichukuliwa juu na malaika mpaka kifuani mwa Ibrahimu.

Kifuani mwa Ibrahimu ndio peponi kwenyewe kwa lugha nyingine, ni mahali pazuri sana, ni sehemu ya mbingu japo sio kule mbinguni kabisa Mungu alipo, ni sehemu ya kitambo tu ambapo watakatifu wanahifadhiwa wakisubiria siku ile ya Unyakuo ifike warudi makaburini kuichukua miili yao, na kwa pamoja sasa waungane na wale watatakatifu ambao watakuwa hai wakati huo, kisha wote kwa pamoja wapewe miili ya utukufu waende kumlaki Bwana Yesu mawinguni, baada ya hapo safari ya mbinguni moja kwa moja inaanza, kwenda kula karamu ya mwana-kondoo kwa Baba mahali ambapo hakuna hata mmoja wetu amefika kwasasa, huko ndipo tutakapomwona Mungu wetu uso kwa uso..tutaona vitu ambavyo hatujawahi kuona, wala kusikia.

Lakini kinyume chake ni nini kinatokea baada ya kifo kwa mwenye dhambi? ikiwa amekufa akiwa mlevi, mzinzi, muuaji, mtukanaji, yaani kwa ufupi yupo nje ya Kristo, basi wale malaika ambao Mungu aliwaandaa kwa kazi ya kuyatenga magugu na ngano (waovu na wema) wanafanya kazi yao hapo, wanamchukua na kumshusha kaburini (kuzimu).

Mathayo 13:49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

50 na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Kumbuka biblia inaposema Mwisho wa dunia inamaanisha mwisho wa aina mbili, aina ya kwanza ni ule mtu anapokufa ndio unakuwa mwisho wake wa dunia, vilevile siku ile ya kiama ambapo dunia yote itahukumiwa nayo pia inaitwa mwisho wa dunia, vyote viwili malaika watafanya kazi hiyo..

Hivyo basi mtu kama ni mwovu, akifa bila kupoteza muda atachukuliwa na malaika hawa na kwenda kutupwa mahali panapoitwa JEHANAMU, au KUZIMU, huko Jehanamu ni mahali tofauti kabisa na ZIWA LA MOTO, Jehanamu ni kama mahabusu, watu waovu wanahifadhiwa kwa muda tu, wakisubiria hukumu ya mwisho, kisha ndio wakatupwe kwenye lile ziwa la moto siku ile ya mwisho.

Sasa huko jehanumu ni mahali pa mateso sana, sehemu mbaya sana, ndio kule Yule tajiri wa Lazaro alipopelekwa

Luka 16.22 “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.

24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.

26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,

28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.

29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu

31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu”.

Huko kuzimu mtu atakaa huko huko katika mateso hayo muda wote huo akisubiria ufufuo ambao utakuja mara baada ya ule utawala wa miaka 1000 kuisha, ndipo atakaposimama sasa mbele ya kiti cha hukumu cha mwana-kondoo kisha atahukumiwa kutokana na maovu yake yote, na kisha kutupwa katika lile ziwa la moto mahali ambapo pana mateso makali sana ya moto usiozimika…Na Baada ya hapo habari yake itakuwa imeisha.(Ufunuo 20:11-15)

Swali linakuja je! Na wewe umejiwekaje tayari ikiwa siku hiyo imekukuta kwa ghafla?, Je! Unao uhakika wa kusikia sauti nzuri za malaika wakikuimbia nyimbo za ushindi wakikunyanyua na kukupeleka kule peponi walipo watakatifu wengine au kuwaona wakija katika hasira kali kukukokota ili kwenda kukutupa Jehanum?. Jibu lipo moyoni mwako.

Kama hujaokoka kweli kweli, Badilika sasa, tengeneza maisha yako kwa Bwana YESU sasa. kwasababu hiyo kesho unayoisumbukia pengine inaweza isiwe yako. Na baada ya kufa ni hukumu.

Lakini pia usisahau tunaishi ukingoni mwa nyakati… Unyakuo umekaribia sana.

 *BWANA YESU ANARUDI.*

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *