“ AKAMWAMBIA, ANGALIA, UMEKUWA MZIMA; USITENDE DHAMBI TENA, LISIJE LIKAKUPATA JAMBO LILILO BAYA ZAIDI .”

Biblia kwa kina No Comments

 

AKAMWAMBIA, ANGALIA, UMEKUWA MZIMA; USITENDE DHAMBI TENA, LISIJE LIKAKUPATA JAMBO LILILO BAYA ZAIDI .

Shalom nakusalimu katika jina la Yesu Kristo karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kwa nini Bwana Yesu sehemu nyingi alizokuwa akiwaponya watu alikuwa akiwaambia wasitende dhambi tena? Na kama wakitenda basi kuna jambo baya zaidi ya lile la kwanza litawapata.

Sasa ni muhimu sana kuwa makini na maneno ambayo Bwana Yesu aliyokua anayazungumza kwa sabababu Bwana Yesu alikuwa hatanii au kumtishia mtu bali alikuwa anasema ukweli na kama tukiwa makini yako mambo mengi sana ambayo tunaweza kuyaelewa na tukasaidika katika sehemu kubwa sana katika maisha yetu ya wokovu.

Ni vizuri kufahamu watu ambao tumeokoka tunawindwa sana na shetani kwa lengo la kuangushwa na kurudi nyuma kabisa katika maisha yetu ya wokovu hivyo tuko vitani na kama tuko vitani basi inatupasa kuwa makini na kuwa waangalifu sana. Maandiko yanasema..

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Unaona hapo? Paulo hasemi “ Kwa maana kushindana kwangu ” bali anasema “ kwa maana kushindana kwetu  maana yake anaonyesha kila Mkristo aliyeokolewa kutoka dhambini(sio yeye mhubiri tu) yupo katika mashindano/vita na si vita vya mwilini bali vita vya rohoni na hapa wakristo wengi ndio wanashindwa kuelewa wanataka vita vya rohoni wanataka vihamie mwilini jambo ambalo haliwezekani.

Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu anaonyesha vita vyetu ni “ juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Sasa nataka turudi kwenye ujumbe wetu kwa nini Bwana Yesu anawaonya watu wale aliokuwa anawaponya kuwa wasitende dhambi tena yaani “ wasiendelee kuishi katika maisha ya dhambi” au wasiizowelee dhambi.

Dhambi ndio inayofungua milango/inayokaribisha mapepo katika maisha ya mtu dhambi ndio inayosababisha watu kuwa mbali na uso wa Mungu, hivyo mlango mkuu wa mapepo na mambo yote mabaya ambayo yanampata mtu chanzo chake kikubwa ni dhambi (simaanishi hata mtu anaepitia katika majaribu kwa ajili ya kupiga hatua katika roho basi naye ni dhambi Hapana)

Maandiko yanaposema…..

Waefeso 4:27”wala msimpe Ibilisi nafasi.”

Sasa tunampaje nafasi Mtume Paulo anaelezea katika mstari unaofata……

Waefeso 4:28 “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.”

Unaona hapo anavyosema? _Mwibaji asiibe tena maaan yake mzinzi asizini tena, muongo asidanganye tena, mtukanaji asitukane tena,mtu mwenye wivu asitawaliwe na wivu tena nk.

Sasa leo hii watu wengi wanakimbilia kuombewa,kupata mafuta ya upako,maji nk vile vitu kweli huenda vikawa vimeombewa kabisa na huenda vikawa na nguvu ya Mungu kwa ajili ya kuwaponya watu au kuwasaidia watu.

Lakini je? Watu wale bado wanaendelea na mtindo ule ule wa maisha walionao? Yaani bado wanaishi dhambini nk ndio maana watu hao hali zao huwa zinazidi kuwa ni mbaya kwa sababu bado maisha yao yanampa nafasi shetani.

Sasa Bwana Yesu anasema kitu kimoja kikubwa sana naomba tukitafakari kwa Pamoja kwa ufupi sana.

Mathayo 12:43-45 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, AKITAFUTA MAHALI PA KUPUMZIKA, ASIPATE.

[44] Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata AKIJA, AIONA TUPU, IMEFAGIWA, NA KUPAMBWA.

[45] MARA HUENDA, AKACHUKUA PAMOJA NAYE PEPO WENGINE SABA WALIO WAOVU KULIKO YEYE MWENYEWE, NAO HUINGIA NA KUKAA HUMO; NA MTU YULE HALI YAKE YA MWISHO HUWA MBAYA KULIKO YA KWANZA.

Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.”
Nataka tuone huo mstari wa 43 vizuri anasema
“…AKITAFUTA MAHALI PA KUPUMZIKA, ASIPATE.”

Kumbe pepo linalotoka ndani ya mtu huwa linatafuta mahali pa kupumzika maana yake kukaa(makazi) lakini Pamoja na kutafuta kote sehemu zote huwa halipati.

Sasa lisipopata ni nini kinachoendelea ndio hapo anasema Master Jesus huwa pepo linafanya kazi ya kurudi na kuangalia mara kwa mara yaani siku kwa siku kwa hiyo likikuta mlango ule umefunguliwa linachofanya ni Kwenda kuita pepo wengine saba wenye nguvu zaidi yaani ili lijihakikishie ulinzi pale linapofanya kazi yake lisiwe na wasiwasi wa kutolewa kabisa na hayp mapepo mengine yaliyoletwa yanazidi kumtesa mtu na ndio maana hali ya huyo mtu huwa ni mbaya kwa sababu mapepo saba yote yanakua yanafanya kazi tofauti tofauti katika mwili wake.

Hivyo ndugu yangu usiruhusu kabisa maisha ya dhambi katika maisha yako yaani namaanisha kuzoelea maisha ya dhambi kuwa comfortable dhambini na ukaona ni kawaida tu hiyo ni tiketi ya mapepo kuanza kukusumbua na kukuangusha kabisa katika maisha ya kiimani, unapoona

Dalili moja yapo ambayo inabidi uwe nayo makini ni pale unapoona yale ambayo uliyaacha baada ya kuoka umeanza kuyarudia tena basi jua kabisa kuna namna hauko sawa simama imara na uendelee mbele usikubali kurudi nyuma kata namna yeyote Kristo yuko Pamoja na wewe na anakupenda sana.

Mungu akubariki sana.
@Nuru ya upendo
Mawasiliano:0613079530
MT Paul

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *