
USIDANGANYWE NA DHAMBI
Waebrania 3:12-13 “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
[13]Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa UDANGANYIFU WA DHAMBI.
Dhambi huwa inadanganya, inaweza ikakuahidi kuwa utapata mafanikio baada ya kuiba, baada ya kusema uongo, baada ya kupokea rushwa, au utapata raha baada ya kufanya uasherati lakini kumbe mwisho wake unapokea mshahara wa mauti.
Siku zote fahamu hilo, kwamba ukifanya dhambi yoyote ambayo unajua kabisa ni dhambi lakini dhambi inakudanganywa kufanya, fahamu kuwa lazima tu utapokea malipo yake, kuna vitu tu lazima vitakufa ndani yako…amani, upendo, furaha n.k vitakufa kidogo kidogo, lakini pia hata vile vya nje vitakufa… mahusiano yako ukiwa umeoa au umeolewa, kazi, elimu, afya, n.k vitakufa.
Unaweza usione matokeo wakati huo huo lakini mbeleni utaona tu. Kwani dhambi inatabia ya kukudanganya kuwa hamna shida lakini kumbe mwisho unaenda kufa kabisa..na ni heri hata ingekuwa unakufa kwa habari ya vitu hivyo tu, lakini pia kuna ile mauti ya pili yaani hilo ziwa la moto. (Ufunuo21:8).
Usidanganywe kuwa ukifa katika dhambi utaenda kuokoka kule, baada ya kufa ni hukumu…unashuka kuzimu mahali pa mateso, kisha baadaye unakuja kutupwa kwenye ziwa la moto.
Hivyo tukae mbali na dhambi zote za mwilini na rohoni. daima Kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23), usikubali kabisa kudanganywa na dhambi.
Kumbuka hata kujipamba kwa mapambo ya nje ni dhambi (1Petro3:3), hata kuvaa vimini, nguo za kubana, suruali kwa mwanamke ni dhambi (kumb22:5 & 1Timotheo2:9), kunyoa denge/kiduku ni dhambi (Walawi 19:27), kusuka, kupaka kucha rangi ni dhambi.
Lakini pia kuwa na mahusiano ya kisiri siri, au ya wazi kinyume na utaratibu wa kiMungu ni dhambi, kusikiliza miziki ya kidunia, kutazama filamu zenye maudhi ya kidunia, kutazama pornography, kushabikia mpira, kubeti, kucheza magemu, kuchora mwili vyote ni machukizo kwa Mungu na ni dhambi kama dhambi zingine tu.
Kuchukia ndugu yako au mtu yoyote ni dhambi pia, kusengenya, kunung’unika, kulaumu laumu, kuwaza vibaya, kujiona bora kuliko wengine/kiburi, vyote ni dhambi na dhambi zote mshahara wake ni mauti tu.
Bwana atusaidie.
Je umempokea Yesu ipasavyo? Fahamu kuwa huwezi kushinda dhambi kwa nguvu zako mwenyewe. Unahitaji kumpokea Yesu akupe nguvu ya kushinda dhambi zote.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.