TAFUTA VAZI LA ARUSI UNYAKUO UPO KARIBU! Awali ya yote tukumbuke kuwa lengo la kunyakuliwa sisi ni ili kwenda kula karamu ya arusi ya mwanakondoo mbinguni, aliyoiandaa Yesu Kristo kwa ajili yetu, kama alivyosema katika Yohana 14:1-4 na Ufunuo 19:9. Hivyo kama tunavyojua hakuna sherehe yoyote isiyokuwa na mwaliko. Hakuna mtu anayejikuta tu kwenye arusi ..
Archives : April-2026
LAKINI USIKU WA MANANE PAKAWA NA KELELE. Kama wewe ni mfuatiliaji wa unabii wa biblia na mwenye kujua nyakati na majira tunazoishi…basi bila shaka unajua kuwa kuja kwa Bwana wetu YESU KRISTO kumefananishwa na wale wanawali kumi waliokuwa wakingoja kumlaki Bwana wao atakapokuja waende naye arusini, Na tukisoma tunaona ilipofika usiku wa manane wote waliishiwa ..
SI KWA NGUVU ZETU WENYEWE!! Shalom mtu wa Mungu, ni siku nyingine tumepewa neema ya kuishi, Hivyo karibu kwa pamoja tushiriki kujifunza maneno ya uzima, ambayo ndio msingi hasaa wa sisi kuwa hapa duniani. Wapo watu wanashangaa inawezekanikaje mtu aliyezaliwa mara ya pili kuishi bila kuzini, mtu kuishi bila kutazama pornography, kuishi bila pombe, kuishi ..
LAKINI WAKATI WA TAABU WATASEMA SIMAMA, UTUOKOE. Ulishawahi kuwa na watu ambao wanakutafuta tu wakati wa shida ili uwasaidie..kisha baada ya hapo hawana habari tena na wewe, mpaka tena wapate shida wanakutafuta, kama ndio, basi kuna hali Fulani ulijisikia ambayo sio nzuri, ni kweli wapo ambao mazingira yanawabana washindwe kukutafuta nyakati nyingine, lakini wapo ambao ..
WAMENIACHA MIMI NILIYE CHEMCHEMI YA MAJI YA UZIMA, WAKAJICHIMBIA MABIRIKA YAO. Yeremia 2:13 “Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji”. Ipo tofauti kati ya chemchemi na birika, chemchemi ni chanzo cha asili ambacho hutoa maji yake yenyewe, haihitaji kuchimbwa, ..
TATIZO LA WATU WENGI LEO!! Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe sana. Karibu tujifunze Biblia, leo kwa Neema za Bwana tutajifuza juu ya Namna ya kutoka katika uvuguvugu wa kidunia. Huwa inauma sana unapokutana na mtu na unamwuliza umempa Bwana maisha yako na anakujibu NDIO, na unaendelea kumwuliza je! Bwana akija leo una uhakika ..
HATARI YA KUWA VUGUVUGU. Bwana Yesu alisema kupitia Mtume Yohana.. Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI, WALA HU MOTO; ingekuwa HERI kama ungekuwa baridi au moto16 ..
KILA MMOJA WETU ANAWAJIBU WA KUMTUMIKIA MUNGU. Watu wengi wanadhani kumtumikia Mungu ni kazi ya watu Fulani, labda walioitwa mahususi kwa ajili hiyo. Na wengine wanafikiri hawawezi kumtumikia Mungu kutokana na sababu mbali mbali, mfano kutokuwa na elimu ya kutosha, kutokuwa na fedha, au kwasababu ya udhaifu waliyonayo. Lakini leo natumai utapata kitu katika somo ..
FUNGA KWA NAMNA HII ILI UPATE KILICHO BORA ZAIDI. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lisifiwe daima. Karibu tujifunze habari za ufalme wa Mungu. Kama tunavyojua zipo gharama za kutafuta kitu, katika maisha ya kawaida hakuna mtu yeyote anayetafuta elimu ya kidunia katika hatua za awali akajihusisha na mambo ya ulimwengu huu, kwanza kabisa wengi ..
TUNATAZAMIA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA 2Petro 3:13 “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”. Ipo mbingu mpya na nchi mpya ambayo wana wa Mungu wameandaliwa, ni nchi ya raha ya milele. Isaya 65:17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya ..