USINYWE MAZIWA TENA!!

Biblia kwa kina No Comments

USINYWE MAZIWA TENA!!

1 Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.

[2]Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,

[3]kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?

Vitu vinavyodhoofisha ukuaji wa kiroho ni pamoja na kutokuwa mwombaji, kutosoma na kujifunza Neno la Mungu, kutowashudia wengine, kutokuwa mtu wa kufunga mara kwa mara, kutojikana nafsi, kutojitenga na makundi mabaya na marafiki wa kidunia, kutazama na kusikiliza vitu visivyofaa mfano miziki ya kidunia, filamu zenye maudhui ya kidunia, picha chafu, kushinda mitandaoni kufuatilia vitu visivyojenga roho, kufuatilia mafundisho manyonge yanayohubiri tu mambo ya duniani, kusongwa na kazi sana,

Rekebisha moja ya sehemu hizo ili ukue kiroho usiendelee kunywa maziwa kila mwaka!! Na utajuaje wewe ni mchanga kiroho? Kwa kuwa na tabia za mwilini!!

Tabia za mwilini ni kama husuda/wivu, ugomvi, fitina, kiburi, chuki, kutokusamehe, vinyongo, visasi, mashindano yasiyojenga, kuwa na hofu iliyozidi mfano kuogopa wachawi, kuogopa mapepo, kuogopa wanadamu, kutomwamini Mungu ni tabia za mwilini pia.

Bwana atusaidie tuwe watu wa rohoni na tukue kila siku.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *