MTU ASITAFUTE FAIDA YAKE MWENYEWE.

Biblia kwa kina No Comments

Hands giving & receiving money – United States Dollars (or USD) bills

MTU ASITAFUTE FAIDA YAKE MWENYEWE.

1 Wakorintho 10:24 “Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.”

Kutafuta faida yako mwenyewe ni ubinafsi!!, na hili jambo limekuwa la kawaida sana ndani ya kanisa la Mungu, lakini ni jambo linalomhuzunisha Mungu. kuwa mbinafsi tafsiri yake ni kutokuwa na upendo…na maandiko yanasema pasipo upendo sisi sio kitu na hutuwezi kumuona Mungu.

1 Wakorintho 13:1-7 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

[2]Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

[3]Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

[4]Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

[5]haukosi kuwa na adabu; HAUTAFUTI MAMBO YAKE; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

[6]haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

[7]huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

Ubinafsi ni tabia ambayo kila mtu aliyezaliwa anayo, lakini mtu akishazaliwa mara ya pili anapaswa kuacha hiyo tabia ya ubinafsi. Na utajuaje kuwa we ni mbinafsi? Pale unapotanguliza kwanza mambo yako zaidi ya wengine, pale unapotafuta kwanza faida yako na mwingine baadaye, pale unapojali kwanza tumbo lako zaidi ya wengine, pale unapotunza vizuri mwili wako kwa kuvaa nguo ya thamani na hapo kanisani kuna mtu amevaa kiatu kilichotoboka, na wewe hata hujali!!, jirani yako anakaa kwenye nyumba inayovuja lakini wewe unakaa katika ghrofa,

Lakini pia hata kujua maarifa ya ki-Mungu na hauwashirikishi wengine..ambao wanaangamia kwa kukosa maarifa huo pia ni ubinafsi, kutowahubiria wengine ni ubinafsi, kwenda kanisani mwenyewe bila kualika majirani ni ubinafsi, kuwa na desturi ya kujiombea kwanza ndio wengine wafuate ni ubinafsi…ndiyo kuna wakati utajiombea wewe binafsi, lakini isiwe desturi..penda kuwatanguliza wengine, kuna mtu anajua biblia yote lakini hajawahi hata kuwashirikisha wengine alichokijua huo ni ubinafsi…yaani kutaka kwenda mbinguni mwenyewe ni ubinafsi, ukiokoka unapaswa uwahubirie ndugu zako, majirani zako nao waokoke…wakikataa unazidi kuwaombea.

Wafilipi 2:4-5 “Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

[5]Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

Tabia ya ubinafsi ni tabia ya kidunia, sisi kama wana wa nuru hatupaswi kuwa na hiyo tabia, tuwachie watu wa dunia.

Bwana Yesu atusaidie.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *