
LAKINI KWASABABU YA ZINAA
1 Wakorintho 7:1-2 “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
[2]Lakini KWA SABABU YA ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake MWENYEWE, na kila mwanamke na awe na mume wake MWENYEWE.
Neno la Mungu linatuelekeza tukimbie zinaa (1Wakoritho6:18), kukimbia zinaa pia ni pamoja na kuwa na mke/mume wako mwenyewe. Ukiona huwezi kujizuia na uasherati ambayo inajumuisha kutazama pornography, kujichua, kujisaga, kuwaka tamaa mara kwa mara, ni heri uoe/uolewe.
Lakini hii haimaniishi ukioa au ukiolewa ndio umeshinda uasherati wa kujichua, uasherati wa kutazama picha za uchi na kutamani tamani kila wakati, hapana!! kama hujaokoka kweli kweli na kujazwa Roho Mtakatifu bado uasherati utakuwa pale pale. Utaoa lakini bado utajichua kama kawaida, utaolewa lakini bado utaendelea kutazama video za ngono na kujisaga kama kawaida.
Kwahiyo kwa ufupi lengo kuu la kuoa au kuolewa sio kuokoka na uasherati, bali mtu anapaswa kuokoka kwanza yaani kuacha uasherati na dhambi zote kabla hata hajafikiria kuoa au kuolewa!!, kuoa na kuolewa ni moja ya sehemu ndogo ya kumuepusha mtu kuanguka katika zinaa. Kwa mfano badala ya kuelekeza macho yako kwa wanaume au wanawake wa watu au vijana na mabinti ambao hawajaolewa, sasa unaelekeza macho yako kwa mume wako/mke wako peke yake, mawazo yako unapeleka kwa huyo tu peke yake na sio wengine…hapo utakuwa umejiepusha na zinaa,
Je! Umeokoka ipasavyo?? Ukiona bado nguvu ya dhambi ipo ndani yako, huwezi kujizua na uasherati..kila ukiwaka tamaa unaenda kujichua, ukiona huwezi kukaa bila kutazama hizo picha za uchafu, basi hapo unahitaji kuchukua uamuzi wa kuokoka kweli kweli na kuacha huo uchafu, na Mungu atakupa nguvu ya kushinda dhambi zote, na utaishi maisha ya raha na uhuru.
Bwana Yesu akubariki.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.