
MAMBO AMBAYO JICHO HALIKUYAONA WALA SIKIO HALIKUYASIKIA
1 Wakorintho 2:9 “lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Kuna mambo ambayo tumeandaliwa na Baba yetu wa mbinguni, mambo mazuri ambayo jicho halikuwahi kuona wala sikio kusikia, kama umewahi kuona mambo mazuri hapa duniani au umewahi kufurahishwa na jambo fulani nzuri hapa duniani, basi siku ile tutakapokaribishwa katika makao yetu.. tutaona na kustaajabia mambo ya ajabu, mambo ya kufurahisha na kushangaza mno, tutaona mazingira ambayo hatujawahi kuona, tutashangaa kuona vitu ambavyo hatujawahi kuona, mambo hayo hatuwezi kustahimili kuona kwa sasa tukiwa na miili hii ya unyonge.. lakini siku ile tutakapovikwa miili ya utukufu tutanyakuliwa na kupelekwa juu sana..huko ndiko kuliko na mambo mazuri ya ajabu sana. Ukijua hayo hautaona ugumu wa kuacha uzuri wa dunia hii ambayo inaharibika na kukaza mwendo katika safari ya Imani, ukijua kuna mambo mazuri yameandaliwa kwa ajili yako.
Kumbuka mambo hayo yasiyoelezeka uzuri wake.. Mungu amewaandalia WAMPENDAO na si kila mtu tu ambaye anajihita mkristo, ni wale tu watakaoshinda, wale waliokataa maisha mabovu ya hii dunia, wale wasiopenda maisha yao katika huu ulimwengu ulioharibika, wale walioacha udunia na kumfuata Bwana Yesu kweli kweli..hao ndio Baba amewaandalia mambo ambayo jicho halikuwahi kuona. Lakini kwa wale wanaoipenda dunia, wanaojifurahisha katika anasa na starehe za dunia hii, wale wakristo feki wanaotumia jina la Bwana kustiri maovu, nao wameandaliwa mateso ambayo jicho haljawahi kuona, wameandaliwa dhiki kuu.
Tujiulize je mimi na wewe tumeandaliwa nini? Bila shaka mioyo yetu tunaijua!! Hebu sasa tuchunguze njia zetu na kuzitengeneza sawa sawa…kwani tupo ukingoni sana.
UNYAKUO UMEKARIBIA SANA!!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.