Neno KASIRANI Lina maana Gani kwenye Biblia ( Kutoka 23:21)

  Maswali ya Biblia

Bwana Yesu kristo Asifiwe,

SWALI: Nini maana ya Kumtia Mtu au Malaika “KASIRANI” kama ilivyotumika katika (Kutoka 23:21)

Kwa majibu sahihi turejee biblia katika
Kutoka 23:20-22
[20] Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.

[21] Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; WALA MSIMTIE KASIRANI; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.

[22] Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.

Kumtia Mtu  kasirani ni kumfanya  akasirike
Hivyo Biblia inapowaamuru wasimtie malaika kasirani Ina maana “wasimkasirishe” maana hatowasamehe

JE ni vitu Gani hivyo ambavyo vingemtia Malaika kasirani?
Naam si vingine bali ni “kumwacha Mungu na Kuabudu Miungu mingine migeni pamoja kutoliishi neno lake”
Lakini mara kadhaa tunaona jinsi Wana wa Israeli walivyokuwa wanamtia malaika yule kasirani walipokuwa jangwani hata katika nchi ya Ahadi.

Jambo dhahiri lililoonesha Kumtia malaika yule kasirani ni pale Wana wa Israeli wanapochelewa kuyaondoa yale mataifa yaliyokuwa katika nchi Ile ya Ahadi, Isitoshe hata kufanya agano na miungu yao! Jambo hili ni linafanyika kuwa chukizo kubwa mbele za Mungu na malaika wake Aliyempeleka awaingize katika nchi hiyo ya Ahadi

Waamuzi 2:1-5
[1] Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;

[2] nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?

[3] Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.

[4] Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia.

[5] Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia Bwana sadaka huko.

Hata hivi Leo kuna watu wanawatia kasirani malaika wa Mungu!
Maana imeandikwa Kila mtu aliyeokoka anaye malaika wake ambao hupeleka habari zake njema mbele za Mungu, Sambamba na kumhudumia (mathayo 18:10, Ebrania 1:13-14)
Hivyo tunapoyafanya yaliyo machukizo mbele za Mungu tunawahuzunisha pamoja na kuwatia kasirani Malaika na Mungu wetu.

Kama Wana Israeli walivyomtia Mungu kasirani wakiwa Jangwani, Vivo hivyo hata sisi Leo kwa maasi yetu tunamfanyia kasirani BWANA MUNGU wetu

Kumbukumbu la Torati 9:7-9
7 Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana

8 Tena mlimkasirisha Bwana katika Horebu, Bwana akakasirika nanyi hata akataka kuwaangamiza.

9 Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano Bwana alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.

Unaweza kusoma zaidi katika kumbukumbu 31:29

Mungu atusaidie kuyafanya yaliyo mapenzi yake bila Kumtia kasirani

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT