Biblia inaposema kila apitaye cheo hana Mungu (2Yohana 1:9 ) inamaana gani?

  Maswali ya Biblia

JIBU, Tusome

Cheo’ maana yake ni ‘kipimo’
Mfano mtu mwenye kipimo kikubwa kazini au katika eneo fulani maana yake mtu huyo ana cheo kikubwa katika hiyo kazi au hilo eneo.. Wakati mwingine mtu mwenye heshima zaidi ya wengine serikalini au kwenye mamlaka fulani mtu huyo ana cheo kikubwa..

Marko 6:21
[21]Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;

Hata mtu mwenye umri mkubwa tunaweza kusema ana cheo kikubwa cha umri..

Mwanzo 43:33 “Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao”

Sasa tukirudi kwenye Swali, biblia inaposema mtu apitaye cheo ni mtu wa namna gani?Kutokana na hilo andiko biblia inatuambia mtu huyo ni yule aliyevuka kipimo au mipaka ya mafundisho ya neno la Mungu.Kwa mfano, neno linasema usiibe au usizini mtu huyu anatafuta njia ya kuhalalisha wizi au uzinzi…

Mtu huyu anajua kabisa kitu fulani ni dhambi lakini anataka kuifanya ile dhambi ionekane kitu cha kawaida ili afanye atakavyo. Mtu wa aina hii ndiye aliyevuka cheo cha mafundisho ya neno la Mungu, yaani alikuwa katika njia nzuri ila anaanza kuvuka ile mipaka ya neno. Maandiko yanasema mtu wa namna hiyo hajamuweka Mungu ndani yake.Kwa jinsi hiyo ni muhimu sana kuisimamia katika neno la Mungu maana tayari limehakikiwa halihitaji marekebisho yoyote yatupasa tuliishi kama lilivyo..

Mithali 30:5-6[5]Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.[6]Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.

Tukienda zaidi ya kipimo (cheo) kutokana na tamaa zetu za kufanya mambo maovu, tukaligeuza neno la Mungu tuwe na uhakika hukumu inatungoja kama ilivyoandikwa katika

Ufunuo 22:18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki”

Tumuombe Mungu atuwezeshe kufikia cheo na si kukivuka Waefeso 4:14

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT