Fahamu maana ya Nardo ,Yohana (12:3).

Maswali ya Biblia No Comments

Nardo ni moja ya mmea mdogo sana unaojulikana kama”Nardostarchy” mmea wa aina hii huwa inatoa maua madogo madogo yenye rangi ya pinki Pia mmea huu huwa na vijitunda vyeusi ambavyo ndio chanzo cha mafuta ya aina ya nardo ambayo hutumika kutengeneza madawa asilia pamoja na marhamu safi yaani kwasasa huitwa Perfume (marashi/manukato)ambayo ndio huwa na gharama kubwa zaidi kuliko zingine.Tuone katika pia Biblia inazungumzia huu mmea.

Tusome katika Yohana 12:3

3 “Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya NARDO SAFI yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.

4 Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,

5 Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa DINARI MIA TATU, wakapewa maskini

”Hivyo Pafyumu(manukato)yaliyotengenezwa kwa “Nardo”, yalikuwa ni yenye gharama kubwa sana na hata sasa ni ya gharama kubwa kutokana na upatikanani wa mmea huo.

Mimea jamii ya “ Nardostachy” ni mimea ambayo inapatikana katika safu za milima ya Himalaya iliyomo nchini Nepali . Na pia baadhi ya maeneo machache nchini india pamoja na China.

Mazingira ya ukuajie wake huwa inaanza kumea kuanzia kimo cha mita 3000 mpaka mita 5000 kutoka usawa wa bahari(Mita 5,000 ni karibia na urefu wa mlima kilimanjaro) . Hivyo kupelekea upatikanaji wake kuwa ni mgumu sana, kutokana na uchache wa maeneo mmea huu unapomea na kukua. Kwasababu hiyo inapelekea marhamu ya Nardo kuwa na gharama kubwa zaidi.Mpaka hapo tutaona kuwa marhamu alipakwa Bwana Yesu Na yule Mwanamke ilitoka mbali na ilikuwa na Gharama kubwa Mno sawa na dinari 300 ambayo ni sawa na milioni 6 za kitanzania Mistari mingine inayozungumzia Marhamu ya Nardo ni pamoja na Wimbo ulio bora 1:12, na 4:13-14

Bwana Yesu akubariki Shalom. 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *