Fahamu maana ya “sayuni”.

Maswali ya Biblia No Comments

SAYUNI, katika Biblia tunangalia mwanzoni kabisa ambapo Daudi  alipokwenda kuuteka Mji wa Yerusalemu  na akafanikiwa .. Eneo lile alililoliteka liliitwa ngome ya SAYUNI.  Tutaona katika kitabu cha (2Samweli 5:7).

Sasa cha kufahamu ni kwamba  katika maandiko Sayuni  imetumika nakutambulika kama mji wa Daudi au Mji wa Mungu(YERUSALEMU)..    Pia mahali pa mlima ambako hekalu la MUNGU  lilipojengwa lilifahamika kama mlima sayuni ambalo lipo katika mji wa Yerusalemu.

Tutasoma pia katika (Yeremia 31:6,12) kuthibitisha hilo.Mahali pengine ambako biblia imetaja Sayuni kama watu wa Mungu yaani wayahudi ni katika kitabu cha (Isaya 60:14)

Isaya 60:14 “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako [Israeli] na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli” Unaweza kuona hapo.

Kadhalika ukisoma pia (Zakaria 9:9, Sefania 3:14-19),biblia inamtaja Israeli kama binti Sayuni. Haya yote yanaonyesha pia Wayuhudi mbele za Mungu ni sawa na SAYUNI yake. Hata hivyo pia i katika agano jipya neno Sayuni linatambulika  kama ufalme wa watu wa Mungu wa rohoni.

Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,”

Hapo Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu  anaonyeshwa Sayuni  ambayo Mungu aliikusudia kwa watu wake wanaomfuata na kuzishika amri zake tangia zamani yaani hiyo Yerusalemu ya mbinguni kanisa la Mungu. Hata hivyo Mtume Petro pia aliandika katika…

1Petro 2: 6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate  hayo.”

Kwa hiyo  maandiko hayo nayo yanathibitisha kuwa kanisa ndiyo Sayuni ya Mungu na ndio pia Yerusalemu ya mbinguni,..na tunapaswa kufahamu  kuwa Kanisa msingi wake ni Yesu Kristo, na vilevile kujua kuwa hiyo Sayuni pia ni jiwe kuu lake la pembeni linaonekana ni YESU KRISTO BWANA WETU. Kwahiyo na sisi pia tujitahidi kwa bidii bila kukata tamaa tuwe  pamoja na Bwana Wetu Yesu kristo  katika SAYUNI/YERUSALEMU mpya ya Mungu  ambayo Mungu mwenyewe alishakwisha kuanza kuiandaa na anaendelea kuiandaa hapa duniani .

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *