Nini maana ya Uru ya ukaldayo?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu,Tusome pamoja…

Mwanzo 11:28-29[28]Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.

[29]Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska

Neno hili Uru, lina maana ya ARDHI,AU HIMAYA, Na hapo maandiko yanaposema Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika URU wa Wakaldayo”, inamaanisha Tera alikufa kwenye ardhi au himaya ya wakaldayo..

Lakini tukiangalia kimaandiko tunaona zilikuwepo huru nyingi,zamani za kale,huru za waashuru na waajemi japo iliyotajwa kwenye biblia tunaona ni huru ya wakaldayo tu..

Na tunaona Abrahamu aliambiwa atoke kwenye nchi aliyozaliwa,ambayo ndio huru ya wakaldayo aende nchi nyingine asiyoifahamu,

Hii ikituonyesha Mungu anapomwita mtu anapaswa atoke mahali alipo na kwenda sehemu nyingine kiroho..

Mwanzo 12:1-3[1]BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

[2]nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

[3]nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa…

Jiulize toka umeokoka,kwa kumpokea Yesu Kristo Katika maisha yako,umetoka Katika himaya za dhambi na uovu, je umetoka na kujitenga na himaya za ulevi na uzinzi,umetoka kwenye himaya za ushirikina na uganga, ikiwa bado fahamu kabisa bado ujaianza safari ya Wokovu, ,jitenge na mambo hayo na kuianza safari yako ya imani Katika ukamilifu wa Mungu..

Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *