Maana ya Mithali 20:12,Sikio lisikialo na jicho lionalo Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili

  Maswali ya Biblia

Mithali 20:12[12]Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili..

JIBU..

Unaweza kujiuliza, kwanini maandiko yasingesema sikio na jicho Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili, badala yake anasema…

Sikio lisikialo na jicho lionalo Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili,

Hii ni kutuonyesha jinsi gani kazi zao jinsi zinavyoweza kujitegemea, kwasababu sikio haliwezi kuona wala jicho kusikia kwa kuwa kila kimoja kimewekewa mfumo wake wa kufanya kazi Katika upekee, lakini Katika utofauti wao wa kufanya kazi haifanyi wawe na miungu tofauti bali ni Mungu yule mmoja aliyefanya vyote..

Kwa ujumla tunapaswa tuelewe na kufahamu ni Mungu aliyevifanya na kuumba vitu vyote Katika mionekano yake tofauti, mmoja alimfanya hivi kwa asili ya mhindi, mwingine kwa asili ya mwafrika na mzungu, na sio kwamba kuna mapungufu flani Katika jamii hiyo, sivyo bali ndivyo ilivyompendeza watu wake kutokuwa na mionekano inayofanana…

Na ndivyo alivyoweka Katika Kanisa lake, kila mmoja ana karama yake ambayo ndiyo iliyompendeza Mungu awe nayo, Katika Kanisa kuna wainjilisti,manabii, mitume,waimbaji na Katika hao wote bado Mungu ameweka utofauti wa kutokufanana…

Kutokuimba kama mtu mwingine hakukufanyi usiwe na karama ya uimbaji…

1 Wakorintho 12:4-6

[4]Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

[5]Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

[6]Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

Tunapoyaona haya ndani ya kanisa tusianze kunyoosheana vidole na kutoa malaumu, bali tuendeleze kwa bidii kile Mungu alichokiweka ndani yetu kwa kushirikiana na kujengana, ikiwa tupo kwenye safari ya imani,tusitake kufosi mambo yote yaweze kufanana bali tufahamu hili…

Sikio lisikialo na jicho lionalo Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili..

Simama kwenye nafasi yako na utumike hapo kwa bidii na kwa moyo wote,mana vyote Katika yote tunamrudishia yeye Mungu utukufu wote..

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT