Nini maana ya neno ulafi katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Ulafi ni tabia ambayo mtu anakula chakula bila kiasi, kula kwa kupitiliza, na tabia inapozidi hufanya hata kushidwa kufanya maendeo ya kimaisha au kiroho kwa sababu hufanya kila kitu kitakacho onekana mbele ya macho lazima tu atakila sasa hali kama hii ndiyo inajulikana kama ulafi.

Na tabia hii haitokani na Mungu ndiyo maana maandiko yanasema katika

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ULAFI, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

Mara nyingi tabia hupelekea mtu kufanya jambo lolote ilimradi tu yeye ale, iwe uzinzi atafanya, iwe rushwa, iwe kuiba aua kudhurumu nk.. kwa sababu ya kukosa kiasi ndani yake ndiyo hupelekea kufanya matukio haya tena bila shaka lolote, ikiwa tu atakula basi kunamfanya asione shida yeyote

Ndiyo maana hata Esau kilicho mfanya auze uzao wake wa kwanza kwa isaka, ilikuwa kwasababu ya kukosa kiasi ndani yake ikapelekea hata kupoteza baraka za mzaliwa wa kwanza

Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya CHAKUKA KIMOJA”.

Lakini maandiko yanatufundisha nini katika hili

Mithali 23:1 “Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.

2 Tena ujitie kisu kooni, KAMA UKIWA MLAFI.

3 Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila……

6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;

7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. ATAKUAMBIA HAYA, KULA, KUNYWA; LAKINI MOYO WAKE HAUWI PAMOJA NAWE.

8 Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.”

Umeona ulafi si jambo la kulichulia kawaida tu katika maisha ni jambo mbaya sana na linaleta uharibifu mkubwa sana katika maisha, yawe ya kiroho na hata kimwili, ikiwa kama tabia hii haitachukuliwa hatua kwa mtu mwenye nayo ni wazi kuwa atakuwa katika hali mbaya sana, mfano katika maisha ya mwilini utashangaa, mtu hafanikiwa japokuwa anafanya kazi, ana biashara ana faida kubwa lakini kwa sababu ya kukosa kiasi na ulafi kuzidi ndipo hapo kunamfanya awe duni katika maisha yake anashudwa kusomesha watoto, kuhudumia familia nk..,japokuwa pesa anayo.

Na hata kiroho pia kama nako tukiwa walafi kuna vitu ndani yetu vitapungua maandiko yanasema

Mathayo 17:20-21

[20]Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

[21][Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

Ikiwa kama tutakuwa watu wa kula kula kila mara kifunga itaonekana kama kitanzi kikubwa, au mzigo au mateso kwa sababu ya kukosa kiasi, maana kuna mambo mengine hatuwezi kuyaondoa pasipo kufunga na kuomba sasa ikiwa mtu wa kula kila unachokiona ni wazi kabisa maisha yako ya rohoni hayawezi kupiga hatua, maana kama wokovu si kudumaa bali ni kupiga hatua kila sasa ikiwa hata maombi ya masaa 12 unashindwa Je siku tatu kavu utaweza! Jibu ni la hivyo njia ya kuweza kupiga hatua hata kiroho ni kuacha ulafi pia.

Lakini pia si katika kufunga hata katika mambo ya ulimwengu ikiwa umeshaokoka na bado unaendelea kufanya mambo ya ulimwengu huo pia ni ulafi maana umekosa kijizuia huna kiasi umeshakombolewa lakini bado unatamani mambo uliyoaacha mbele za Mungu ni chukizo

Petro 4:3 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na KARAMU ZA ULAFI, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali.

Ni vyema kuepuka jambo hili katika maisha yetu maana kimsingi halina faida yeyote zaidi ya hasara tu, mwombe Mungu ushinde huku nawe ukijitahidi kuiacha tabia hii

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *