Undani wa Mithali 11:26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani

  Maswali ya Biblia

Ili tuweze kuelewa mstari huu tutazame mfano huu ambao ni uhalisia wa maisha ulivyo ambao sasa utatusaidia kuelewa maana ya (Mithali 11:26)

Kuna kipindi baadhi ya mikoa ya Afrika mashariki (Tanzania ) kulitokea shida ya maji, ilifanya watu kutoka umbali mrefu kwenda kutafuta maji ili waweza kufanikisha shughuli zote zinazohitaji maji, lakini sasa katika kipindi hicho cha changamoto ya maji si kwamba khakukuwa na visima la! kuna watu walikuwa navyo visima vyenye maji kabisa,.lakini baada ya kuona tatizo hilo la maji walivifunga visima vyao ili tu wauze maji kwa bei kubwa, na watape faida lakini jambo hili liliwaumiza wengi, lilifanya watu wanung’unike na kutumia sababu ya bei kubwa waliyokuwa wanaukizwa yele maji, sasa jambo hili ndilo linapelekea mtu yule apokee laana badala ya baraka kwa sababu ya kuwanyima watu maji…

Hivyo hivyo katika mambo yote ya mahitaji kwa binadamu iwe chakula, mafuta nk.. ikiwa tu vikizuiliwa kwa siri ili kukomoa watu kwa kuwauzia kwa bei kubwa nako pia wanafananishwa na watu wanyimao hivyo malalamiko yanapozidi ndivyo laaana vinavyozidi kwako kwa watu wanaotenda mambo hayo, lakini ikiwa wataashiria watauza kwa watu ndipo hapo baraka zitakapo wafuata

Mithali 11: 26 “Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake”.

Ni jambo ambalo tunapaswa kuwa nalo makini, unaweza ukaona kwako unapata faida na unafurahia maisha lakini kumbe huku nyuma tayari laana inakutafuna
Ndiyo maana maandiko yanasema

1Yohana 3:17 “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?”

Hata kiroho pia jambo hili au hii tabia ni mbaya, na haswa katika kipindi hiki tulichopo cha siku za mwisho kulingana na maandiko yanabyosema katika kitabu cha

Amosi 8:11-12

[11]Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.
[12]Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione.

Umeona tayari jambo hili lilikwisha kutabiriwa kuwa kitatikea njaa ya kiroho, sasa kutokana na jambo hili wapo viongozi wa kidini ambao wanatumia jambo hili kama fursa, unakutaka wanafanya biashara kwa kuwa wameshakuwa maarufu basi wanauza vitu vya kuwasaidia watu kukua kiroho kwa bei kubwa, mafano vitabu nk..
Sasa hii pia si sawa tunapaswa tungeuke na tutazame neno la Mungu linatuambia nini

Basi tukisha yajua haya yote yatupasa tuwe makini

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT