Nini maana ya mikono iliyotakata 1Timotheo 2:8?

  Maswali ya Biblia

Mikono iliyotaka ni mikono isiyokuwa na hila au dosari yeyote, yaani mikono ambayo ni safi iliyotakata

1Timotheo 2:8 “Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano”

Mikono yenye hila au dosari nyenyewe inakiwaje, tusome

Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.

16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;

17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.

Sawa sawa na andiko hilo tunaona jinsi mikono yenye dosari inavyokuwa, kumbe mikono isiyotaka inatokana na kuwa na matendo mabaya mbele za Mungu, mikono inayomwaga damu, inayotoa rushwa na kupokea rushwa, inayodhurumu nk.. kwa ufupi tabia kama hizi zipo kwa watu ambao bado hawamwamini Yesu Kristo mikono yao inafaninshwa na mikono iliyo na dosari

Sasa hapo akioosema kuwa “Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano”

Ikiwa wewe ni kiongozi unaongoza watu ni muhimu kuhakikisha kuwa mikono yako ipo safi mbele za Mungu, watu wenye uchaji wa Mungu ndani yao, wenye hofu ya Mungu, wasio na hasira, magomvi nk .

Zaburi 58:1-2

[1]Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki? Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?

[2]Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;

Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.

Hivyo tunapaswa kujitazama sana, isiwe tukawa tunafanya kazi ya kuchosha, utashangaa kwanini tunaomba na hatupati, kwanini uwepo wa Mungu hauonekani kumbe tayari tumemuinulia Mungu mikono iliyo na dosari, kwa kulijua hili basi tujirudi tutubu na kukaa katika Hali ya usafi wa moyo

Yakobo 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. ITAKASENI MIKONO YENU, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili”.

Na ikiwa pia bado ujampokea Yesu Kristo maishani mwako basi wakati ni sasa, kwa maana hakuna njia nyingine inayoweza kututakasa maisha yetu zaidi ya damu yake na hii tunaipata kwa kumpokea Yeye maisha mwetu sawa sawa na warumi 10:9

Na Bwana akubariki

kwa kuchukua uamuzi huo .

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT