Maana ya Mshahara wa Mbwa  kumbukumbu 23:8.

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Kama tunavyosoma katika maandiko Neno “MBWA” linamaanisha “Mwanaume anaejiuza au anaeuza mwili wake” mwanaume anaeuza mwili wake aidha kwa wanawake au kwa wanaume wenzake yaani SHOGA.

ukisoma kwenye Biblia ya kiingereza “Amplified Bible ” imeeleza vyema hebu tusome.

Deuteronomy 23:18
[18]You shall not bring the hire of a harlot or the price of a dog (a sodomite) into the house of the Lord your God as payment of a vow, for both of these [the gift and the giver] are an abomination to the Lord your God.

Unaona hapo anasema “A SODIMITE” maana yake “a person who engages in anal sexual intercourse.” Yaani mtu anaejihusisha na mapenzi kinyume na maumbile. Kama ilivyokuwa kwa watu wa sodoma na gomora.

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.

Sasa Mungu alikataza mtu yoyote anaefanya uovu huo fedha yake kuileta madhabahuni pa Bwana aidha mwanamume anaeuza mwili wake au kahaba yaani mwanamke anaeuza mwili wake kwa wanaume sadaka ya watu wa namna hii ni machukizo makubwa mbele za Bwana.

Kama maandiko yanavyotwambia.

Mithali 15: 8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.

Kumbe sadaka ya mtu mwovu si hao pia sadaka ya mwizi,mlevi,mcheza kamari nk ni machukizo mbele za Bwana.

Si kwamba Mungu anavutiwa sana na sadaka za Fedha au mali tunazomtolea wala hapagawishi na wingi wa fedha tunaomtolea la bali Mungu anaangalia kwanza usafi wetu yaani utakatifu tusifikili kumtolea Mungu sadaka nyingi tena zilizotokana na uzinzi,wizi,uporaji,nk ndio tunamvutia Mungu la!,

Ni vyema kufahamu sadaka ya kwanza kabisa inayokubaliwa na Mungu kabla ya zote ni sadaka ya miili yetu yaani usafi na utakatifu mbele zake. Tunapokwenda kumtolea Bwana sadaka zetu bado ni wezi, wala rushwa ,watukanaji, wazinzi,waasherati ndugu fahamu hiyo sio sadaka bali ni machukizo makubwa.

Bwana Yesu mwenyewe ameshakwisha kutwambia na kutonya kabla kuwa

Mathayo 9:13 “Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”.

Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.

Hivyo kitu cha kwanza anachotaka sio sadaka zetu bali ni REHEMA.lakini aliendelea kutwambia hata tunapokuwa na neno la mtu(kupishana kauli au ugomvi) tusiitoe sadaka kwanza mpaka tuhakikishe tumepatana na ndugu zetu hao kisha title sadaka mbele za Mungu,  hivyo nikuonesha Usafi wa ndani na nje ni muhimu zaidi kuliko sadaka zetu.

Lakini kama tunakwenda kuntolea sadaka zetu na hatuna mpango wowote wa kuacha maisha hayo tunajirisha upepo tu kwa wingi wa sadaka tunazomtolea. Maana zitakuwa si kitu kabisa.

Ufunuo 22:14 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya”

Maandiko yanatusisitiza kuwa huko nje Kuna wachawi,Mbwa(Mashoga) nk hivyo wote hao hawatauona ufalme wa Mbinguni watakwenda kuzimu kama wasipoamua kuzitubia na kuziacha njia zao.

Maranatha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT