JE ADAMU NA HAWA WALIKUWA NA UZIMA WA MILELE?.

Biblia kwa kina No Comments

Shalom!, mwana wa Mungu nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tujifunze na kuyatafakari maneno ya uzima.

Swali hili limekuwa likiulizwa mara nyingi sana na wakati mwingine ni kama vile linakosa majibu.
Ni swali ambalo lina watu wanaokubali ndio Adamu na Hawa walikuwa na uzima wa milele. Lakini kuna kundi lingine linalokataa kuwa Adamu na Hawa hawakuwa na uzima wa milele. hivyo inapelekea kuleta mkanganyiko mkubwa. Lakini leo tutakwenda kutazama kwa usahihi na kwa msaada wa Roho Mtakatifu na hakika tupata majibu yaliyo sahihi.

Sasa je ni kweli Adamu na Hawa walikuwa na uzima wa milele?

Jibu ni NDIO walikuwa na uzima wa milele.
Ni vyema tukafahamu “

Adamu na Hawa Mungu aliwaumba wakiwa hawana dhambi kabisa.” Hawakuwa na aina yoyote ya dhambi na Mungu alipooumba ulimwengu kila kitu alikiona kuwa ni chema kama maandiko yanavyotwambia.

Mwanzo 1:31” Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.”

Unaona hapo!, anasema kila kitu alichokifanya wakati wa uumbaji wake kilikuwa ni chema, hivyo hakikuwa na kasoro yoyote. Mungu anapotengeneza kitu chochote hakutengeneza nusu nusu bali anaumba/kukitengeneza kitu kilichokamilika. Na si hivyo tu anafanya kitu kisichokuwa na kasoro yoyote.


Lakini pia neno la Bwana linatwambia Mungu alimuumba mwanadamu akiwa ni mnyoofu kabisa. Pasipo mapungufu yoyote yale.

Mhubiri 7:29 “Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.”

Na ndio maana Bwana anampa mamlaka Adamu ya kutawala kila kitu duniani maana hakuwa na mapugufu ama kasoro yoyote ile akapewa mamlaka ya kuwa mungu katika dunia hii. kwa kutawala vyote vlivyomo. Maana yake Mungu alimuamini yaani aliiamini kazi ya mikono yake kuwa hakufanya kitu kilicho Nusu.

Swali ? sasa kwa nini Adamu na Hawa walikufa? Kama walikuwa na uzima wa milele je? Walipewa uzima wa milele  nusu?(kitu ambacho hakiwezekani)!

Ili kufahamu hili jambo hebu turudi katika maandiko tusome ili kupata jibu la swali hili.

“Umewahi kufikiri kwa nini Adamu na Hawa baada ya kula tu lile tunda walikwenda kujificha waliposikia sauti ya Mungu?,”

“na kwa nini kipindi hajala lile tunda hakujificha aliposikia sauti ya Mungu?
Je ni nini basi kilichomfanya ajifiche yeye na mke wake?”

Mwanzo 3:8” Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.”


Unaona hapo! Anasema “Adamu na mkewe WAKAJIFICHA kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone”

lakini hapo mwanzo hawakuwa wanajificha wakati ambapo Bwana Mungu wakati wa jioni anaposhuka kuzungumza nao.
Tutafakari tena mfano huu hapa ikiwa hujaelewa vyema hapo juu…

Mwamini yaaani mtu aliemuamini kweli kweli Yesu Kristo anapoanguka katika dhambi ule ujasiri wa kusogea mbele za Mungu huwa unaisha kabisa. Umewahi kufikiri hili jambo? Au wakati mwingine anajiona kama mchafu wala hustahili kusogea mbele za Mungu. Na dhamiri yake inamshudia alichokifanya sio sawa akifanya kwa makusudi au bahati mbaya. Anaona kabisa uwepo wa Mungu ndani yake hakuna anajiona mkavu!.mpaka aombe rehema na toba ndipo ataanza kusikia uwepo unarudi.

Isaya 59:2 “lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

Dhambi ndio iliyomuweka mbali na Bwana ukisoma kwa makini katika kitabu cha mwanzo hapo hatuoni kuwa Mungu ndio alijificha kwa Adamu la! Bali Adamu yeye ndio aliejificha  ili Bwana asimuone kwa sababu ya makosa ama uasi ule alioufanya. Kama maandiko yanavyotuambia hapo juu.

Sasa Adamu alipewa maagizo ambayo kama angelifata basi angeishi na hata leo angelikuwepo! Yaani tungelizaliwa tukamkuta Adamu na Hawa wapo . tusome..

Mwanzo 2:17” walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”

Kumbe uzima wa Adamu ulikuwa katika kutokula ule mti wa matunda ya ujuzi wa mema na Mabaya(Uzima wa Mwamini uko katika Kristo Yesu yaani Neno la Mungu). Yaaani uzima wa Adamu na mke wake ulikuwa katika kulisikiliza Neno la Bwana yaani maagizo yake ama utii wake kwa Mungu.

Maana yake Adamu hakutakiwa kuishi nje ya Neno ambalo ndio Yesu Kristo haleluyaaa!.

Sasa baada ya kukaidi ndio kifo kilipoingia yaani ule uzima wa milele aliokuwa nao ukaondoshwa kwa sababu ipi?? Tusome maandiko.

Warumi 6:23” Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Unaona hapo?! Anasema “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti………”

kumbe hakukuwa na namna Adamu na sisi sote ilitakiwa kulipwa ujira wetu kwa ile dhambi Adamu alioifanya hakukuwa na namna ilibidi afe lakini pamoja na sisi pia watoto wake. Kumbe asingelifanya dhambi wala kusingelikuwa na mauti! “Maana Adamu hakuwa anajua dhambi maana hakuumbwa nayo yeye wala mke wake.”

“Tunakufa kwa sababu ya dhambi maana dhambi ndio iliyoipa mauti nguvu pasipo dhambi hakuna mauti”. Yaani pasipo dhambi mauti haina nguvu yoyote. Nguvu ya mauti iko katika dhambi.

Si kwamba Mungu alikuwa amepanga kumficha Adamu asiijue dhambi la! Alikuwa anampango wa kumfudisha dhambi ni nini na asiifanye katika wakati ambao yeye Bwana ambao alikuwa amekusudia. Maana mwanadamu kwa asili hajaumbwa na Maarifa bali maarifa yanaingia ndani yake taratibu anapokuwa anafundishwa.

“Kama mwanafunzi anaeenda kila siku Shule kufundishwa maarifa ili yakae ndani yake hawezi kufundishwa mara moja tu na akaelewa akawa na maarifa ya kutosha haiwezekani”

Ndio maana Mungu alikuwa akishuka kila siku kuzungumza na Adamu na mke wake yaani kuwafundisha.

Sio kwamba Mungu alikuwa anashuka pale Bustanini na kuanza kupiga story na Adamu na mkewe kwamba wameshindaje, “wameamka salama” au mmekula kisha kisha anaondoka la! Haikuwa hivyo kila siku Bwana alikuwa akishuka kuwafundisha neno la uzima yaani Yesu Kristo.

Lakini Adamu na mkewe hawakuwa ni wavumilivu wakataka kuwahi mbele zaidi na mwisho wa siku maafa yakawakuta.

JE TUNAJIFUNZA NINI JUU YA JAMBO HILI?

Hii inatufundisha pia kwetu sisi wana wa Mungu kama tukitaka kuishi nje na neno la Mungu basi maafa yatatukuta tu, haijalishi tumeokoka lakini tukitaka kutoka nje na maisha ya wokovu hata huu uzima wa milele tulionao tutaupoteza. Salama yetu iko katika Kristo, tusijitumainishe kuishi katika maisha ya dhambi na tunasema tumeokolewa milele Sahau. Yesu hakuja kuokoa mtu halafu aendelee kuwa ni mdhambi la huyo si Yesu aliekufa pale  kalvari. Akaidharau aibu.

Haijalishi kila siku tunalisikia Neno kama Adamu alivyokuwa analisikiliza kila siku jioni lakini bado aliasi vivyo hivyo na sisi tunaweza tukalisikia Neno na bado tukafananishwa na Yule mtu aliejenga nyumba yake juu ya mchanga mvua na pepo zilipovuma zikaipiga nyumba ile nayo ikaanguka tena anguko kubwa.

Yesu hakuja kutoa hakikisho la kufanya dhambi katika wokovu wetu, kwamba hata tukifanya hatutaupoteza LA! ila ametoa hakikisho la kuwa kama yeye(Mathayo 5:33). Fanyia kazi Neno unapolisikia kataa kujitumainisha katika dhambi ndugu utakufa haijalishi Unanena kwa lugha na kutoa unabii, iepuke dhambi kaa nayo mbali kabisa.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *