Katika maandiko bublia inafunua kuwa Bwana Yesu alianza huduma yake akiwa na umri wa miaka 30.
Sasa ili tuweze kujua alikufa akiwa na umri gani, tunahitaji kujua kwanza utumishi wake ulikuwa wa miaka mingapi.
Kulingana na kitabu cha Yohana, Yesu alihudhuria sikukuu tatu za Pasaka, ambazo zilikuwa za mwaka baada ya mwaka. Tukizijumlisha, tunapata jumla ya miaka miwili. Hata hivyo, kutokana na matukio mengi yaliyoandikwa katika Biblia, wanazuoni walikata kauli kwamba kulikuwa na Pasaka nyingine iliyotokea katikati, ambayo ni pasaka.
Kabla ya Pasaka ya kwanza, Yesu alifunga kwa siku 40 jangwani, akasafiri kutoka Yordani hadi Kana na baadaye Kwenda Yerusalemu, akawaita wanafunzi wake, na kuanza kuhubiri. Baada ya kifo na ufufuo wake, aliwatokea watu wengi kwa siku 40 kabla ya kupaa. Huduma ya Yesu Kristo inakadiriwa kudumu miaka Thelathini na tatu na Nusu, kwa kuchukua miaka 30 ya kwanza ikiongezwa hadi miaka mitatu na nusu.
Katika maisha ya Kristo, ni dhahiri kwamba alikufa katika umri mdogo, lakini katika umri huo mdogo, alimaliza kazi aliyoitiwa kufanya duniani. Akiwa mbinguni alionekana kuwa mwanadamu mkuu na mwenye faida zaidi aliyepata kuishi duniani. Hii ni kwa sababu Kristo alithamini wakati wake alipokuwa duniani na alijua kwamba giza litakuja na hangeweza kufanya kazi tena, aliona kazi ya Mungu kuwa chakula chake, kufanya kazi ya Mungu ilikuwa desturi yake kila siku na wakati wote
Tafakari kwa maneno yake mwenyewe aliyoyasema katika vifungu hivi;
Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi”.
Yohana 11:9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu”.
Yohana 4:33 “Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake”.
Kwa ujumla ni kwamba alithamini wakati wake alipokuwa duniani na aliona kazi ya Mungu kuwa chakula chake. Hili lilimfanya amalize huduma yake haraka, bila kusongwa na chochote katika ulimwengu huu.
Tuthamini wakati ambao Bwana ametupa kwa maana wakati wa kumwamini Yesu Kristo ndio sasa. Hivyo mwamini leo ukawe na uwakika umepokea msamaha wa dhambi na uzima wa milele, na baada ya kukamilisha maisha yetu basi jukumu linalofuata ni kuhakikisha tunaukomboa wakati kama vile Bwana wetu Yesu Kristo aluvyoweza kukuomboa wakati na akaleta ukombozi mkubwa nasi hatuna budi kufanya hivyo tukikumbuka kabisa kuwa Dunia tu wasafiri.
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.