Nini maana ya Mhubiri 7:29  “ Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi”.

  Maswali ya Biblia

Mhubiri 7:29  “Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi”.

Uumbaji wa Mungu,alipomuumba Mwanadamu,alimuumba Katika ukamilifu wote, wazazi wetu wa kwanza hawakuwa na kasoro yoyote ya Mwilini hata rohoni, ukamilifu wa kuwa na Amani,furaha, Upendo na kulicha jina la Bwana..

Lakini tunaona ilifika mahali wakaona hayo walioumbiwa na Mungu hayawatoshi wakatamani zaidi ili wawe sawa na Mungu,na ndo hapo wakaanza kubuni namna yao ya maisha watakayoishi..ndo hapo wakashawishwa kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo hapo mwanzo waliambiwa wasile,ili wakipate wanachokitafuta,,, Lakini Mwanadamu mpaka leo hajakipata kile alichokuwa anakitafuta tangu kipindi kile,zaidi ni Matatizo yalizidi kuongezeka ijapokuwa anajitengenezea njia zake mwenyewe ili apate kuishi…

Mambo kama hayo yanaendelea mpaka sasa,tunavyoona watu wakijibadili maumbile yao ili yawavutie watu, mwanamke kujichubua ngozi yake ili tu afanane na wazungu, na kujiongezea make up ili waonekanae wakitofauti, wanadiriki kuweka mpaka kucha za bandia na mawigi, Sasa yote hayo ndio mavumbuzi waliojibunia wenyewe na kibaya zaidi imefika mahali wanabadili maumbile yao kwa kwenda kufanyiwa upasuaji na kupewa dawa zenye kemikali kali, mavumbuzi ya Mwanadamu..

Wameacha kuwa na asili yao ambayo Mungu aliwaumbia nayo wakataka kuwa kama wao wanavyotaka wao, badala sasa mavumbuzi yao waliojibunia yawasaidie lakini kinyume chake yanawaharibu kabisa na kuwapoteza milele..

Hatuna budi kufahamu ni machukizo kwa Mungu kwa sisi wanadamu kujibunia mavumbuzi ambayo yapo kinyume na mapenzi yake, na kuibadillisha miili yetu, kwasababu tokea hapo alituumba kwa mfano wa sura yake Katika ukamilifu wote…Sisi ni kumcha Bwana na kushika sheria na amri zake…

Shalom..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT