Neno ‘bila kazi ya mikono’ linamaanisha nini katika biblia?

  Maswali ya Biblia

Nakusalimu kupitia Jina lipitalo majina yote JINA LA YESU , Karibu katika kujifunza neno la Mungu litupalo uzima wa milele katika maisha yetu.

kuligana na swali hapo, biblia iliposema bila kazi ya mikono, Maana yake ni kuwa kitu chochote kilichotenhenezwa pasipo kitengemezi chochote, kiuhalisi katika maisha yetu, mfano kama mtu anahitaji kitu chochote kwa ajili ya matumizi yake iwe chakula, vitu vya ndani nk. Lazima tu be vitaandaliwa kwa mikono, lakini sasa tunaporudi katika swali maandiko yanaposema bila kazi ya mikono, JE NI KITU GANI HICHO NA KILITENGENEZWA KWA NAMNA GANI HIYO PASIPO KITEGEMEZI CHOCHOTE 

Tusome

Danieli 2:34 “Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande”.

Hapo tunaona mwandishi ambaye ni Danieli, alipewa maono na katika maono hayo aliona jiwe ambalo limechongwa pasipo kazi ya mikono ambalo lilienda likaipiga sanamu, na sanamu hii ni ile aliyoiota mfame Nebukadreza kwa habari nzima kuhusu ndoto ya mfalme Nebukadreza unaweza somo kitabu cha Danieli kwanzia sura ya kwanza.

Sasa jiwe hili lililokuwa linazungumziwa hapo ambalo lilifanyika pasipo kazi ya mikono ikiwa na maana kuwa ni lilijitengeneza lenyewe, LILIMFUNUA BWANA WETU YESU KRISTO, ulikuwa ni unabii wa jinsi Bwana Yesu atakavyo kuja kuharibu na kubomoa falme zote za ulimwengu huu na kusimamisha ufalme wake wa milele, na katika kufanya hili nall wala hatahuitaji msahada wowote, ndiyo maana hata katika kuzaliwa kwake alizaliwa pasipo baba, ndivyo hivyo hivyo na katika kuujenga ufalme wake atafanya mwenyewe, ndiyo maana ya bila kazi ya mikono

Tunajifunza nini katika hili

Yohana 7:7

[7]Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.

Kutokana na mambo mabovu yanayoelendea katika dunia hii ndiyo kitu kitakachofanya Bwana Yesu aje kuuharibu ulimwengu huu kwa sababu hali iliyopo sasa watu wengi wanakana neno la Mungu hawataki kabisa kutii na mwisho wa siku wanasema hayo maneno hayakuuandikwa hayakuwa kwa ajili yetu, ndiyo maana hapo katika maandiko Yesu mwenyewe anasema si kwamba ulimwengu unawachukia ninyi bali unamshukia Yesu Kristo kwa sababu anashuhudia kuwa kazi za ulimwengu ni mbovu, kutokana na watu kutokutii sauti ya Mungu itafanya Dunia hii iharibiwe

Ndiyo maana tunapaswa kuwa makini na watu wa kuukomboa wakati kwa sababu ni kweli utajitumaishia na mambo ya ulimwengu huu lakini mwisho wa siku yataharibiwa jiulize sasa itakufidia nini kwa yote uliyosumbukia kisha yakatoweshwa, suluhisho lipo kwa Yesu pekee ndiyo maana yanasema katika

Luka 12:31

[31]Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.

Hivyo hii ikitukumbusha kuwa sisi hapa dunianj tunapita hivyo basi ni jukumu letu sisi sote kumwamini Yesu Kristo ili atukomboe maisha yetu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT