Maana ya Mhubiri 1:15 “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.

  Maswali ya Biblia

JIBU: Tusome mstari wenyewe.

Mhubiri 1:15 “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.

Ukisoma hapo kwa makini utaona kuna Vipengele viwili,yalipotoka hayawezi kunyooshwa na yasiyokuwapo hayahesabiki…

Tukianza na kipengele cha kwanza, yalipotoka hayawezi kunyooshwa,tufahamu kitabu cha mhubiri kinaeleza juhudi za mwanadamu kutafuta suluhu ya mambo yote yaliyopo duniani kwa nguvu zake mwenyewe bila kumtegemea Mungu wala kumuhusisha, ndo mana tunaona mwisho wa mhubiri ambaye ndiye alijibdiisha kufanya yote anamaliza kwa kusema ni UBATILI mtupu, mambo yote ayawazayo Mwanadamu na hekima yake yote ni ubatili na kujilisha upepo,ambao mwanzoni unaweza kukupa matumaini kwamba unaweza kukufikisha mahali lakini unajikuta galfa upepo umepotea njiani usijue wapi umeelekea, sasa ni sawa ni mwanadamu anayesumbuka na kujihangaisha na mambo Katika huu ulimwengu tunaoishi… 

Aliposema yaliyopotoka hayawezi kunyooshwa, ni kuonyesha kuna mambo ambayo ni makatazo kwa Mungu au hayapo Katika uhalisia wake, au anaweza kuyaweka sawa na kuyafanya yawe yanakubalika kwenye jamii husika, hivyo kwa hekima yake anajaribu aone kama yatakuwa kweli sawa, na hivyo akafahamu kuwa kile kilichokataliwa na Mungu,yaani kupotoshwa hakiwezi kuwa sawasawa,ni kutafuta Matatizo na shida ambazo hazina sababu..

Ndo mana mbele kidogo anasema…

Mhubiri 7:13 “Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?

Tunaona kipindi hiki watu wanatafuta jinsi ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja, wanatafuta sababu ili ionekane ni ndoa iliyokubaliwa na Mungu,na kamwe haiwezi kuwa ni ndoa na hilo linajulikana, imefika mahali mpaka wanabadilisha jinsia zao ili waonekana Wanawake kwa wanaume na, Wanawake waonekana wanaume lakini bado asili ya jinsia zao bado zipo ndani yao,mwisho wake wanajikuta kwenye Matatizo makubwa ya kiafya na wengine kupelekea kufa kabisa…

Hali hiyo ipo kwa wanojulikana kama mashoga wanapojiharibu ili wawe kama Wanawake, wanaharibika maumbile yao hata kupelekea kutokuwa na uhuru wa kukaa na jamii wakijua kabisa ni aibu, kwasababu yalipotoshwa hayawezi kunyooshwa, umeona? zaidi tunawaona hata wale wanaobadili rangi za ngozi zao,unafikiri ni faida gani zaidi wanapata zaidi ya hasara ya Matatizo ya ngozi, kansa na mwisho wa siku ni kupelekea kifo cha mateso..

Ni jambo la kushangaza kuona Wanawake nao wanahalalisha vazi la suruali kuwa ni vazi la jinsia zote, lakini hata wahalalishe kwa muundo gani,kwa kuweka na kupamba kwa matirio za kike kwa namna gani ila suruali itabaki kuwa ni vazi la kiume, kwasababu huwezi kukipotosha kitu alichokinyoosha Mungu ni kupingana na Muumba wako,mwisho wake ni mbaya sana..

Unajipodoa kwa kuweka wanja na kupaka poda na kuvalia mawigi ili uonekane una utofauti na yule ambaye Mungu alikuumba kwa mfano wake, ikifikirie kazi ya Mungu na uache haraka kukinyoosha kile Mungu alichokipotoa…

Hiyo ndo tafsiri ya kifungu hicho..

Kipengele cha pili kinasema,wala yasiyokuwapo hayahesabiki..

Tukiangalia hi dunia,imejawa na mambo mengi ya Mungu, ambayo tunaona Mwanadamu kila siku anazidi kuyavumbua, na takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa ya asilimia 86 ya viumbe bado havijajulikana bado, ingawaje mwanadamu ana muda mrefu..

Mambo mengi yasiyojulikana yamekuwa zaidi ya yale yanayojulikana watu wanaofanya tafiti wanalifahamu hili,kwa kuwa kila siku wanavumbua mambo mapya na kubaki na mshangao, na hiyo inawafanya wawe na ubize wa kutafuta na kuvumbua na kupelekea kusahau mambo yao ya rohoni, na wakiwa na uhakika kuwa itatokea siku watapata jawabu la mwanadamu katika hii dunia…

Ndo mana mhubiri anasema hayo alishayanyia uchunguzi akaona ni UBATILI, kwamba yasiyokuwapo hayahesabiki hata nikiwa na ubize wa mamiaka yote kutafiti milele sitavumbua yote,hakuna tofauti na kuufata upepo, wanadamu saivi wamekuwa bize kutafuta mambo ya duniani kuliko kuutafuta Ufalme wa Mbinguni ambao ndio unadumu milele,ni Jambo la kushangaza kwasababu huwezi kuwambia kitu kwa sayansi yao wanayoiamini…

Mwishoni kabisa mhubiri anatoa hitimisho ya jumla ya mambo yote, anasema,kusudi kuu la mwanadamu kufanya ni KUMCHA BWANA NA KUSHIKA AMRI ZAKE, (Mhubiri 12:13)

Hivyo na wewe pia hakuna sehemu au mahali utaweza kupata jawabu la maisha yako isipokuwa ni kwa YESU KRISTO pekee, huu ulimwengu utakutesa na kukuhangaisha sana, Ukiamua kumpa Yesu Kristo Maisha yako na kumcha yeye,ameahidi kukupa pumziko la roho yako, ndivyo alivyotuhahidi na ahadi zake ni za kweli..

Mathayo 11:28-30
[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.


[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;


[30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Bwana akubariki…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT